Wananchi: Mdahalo umetufunza mengi

Wananchi: Mdahalo umetufunza mengi

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa juzi na ITV umeelezwa kuwa uliotoa mafunzo makubwa kwa watu wengi katika maeneo mbalimbali nchini kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.

Wakati waliohudhuria mdahalo huo Dar es Salaam walikuwa kila mara wanawakatisha watoa mada kwa makofi na vibwagizo vya "CCM, CCM, CCM" na "Babu, Babu, Babu", katika mikoa mbalimbali watu walikusanyika katika maeneo mbalimbali ya vijiweni, baa, madukani kusikiliza huku wengine wakibeba redio na simu za mkononi

Mjini Dodoma, wananchi katika maeneo ya Mitaa ya Nyerere Square, Soko la Dk Rehema Nchimbi na viwanja vya Bunge, walishindwa kuvumilia na kujikuta wapiga kelele za juu katika mada iliyokuwa ikitolewa Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu umuhimu wa kupata Katiba Mpya.

Moshi

Makundi ya wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi wa kawaida walionekana wakifuatilia mdahalo huo uliomhusisha Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wengine.

Wakati mjadala huo ulipoanza tu, watu mbalimbali walionekana kupigiana simu na wengine kutumiana meseji wakihimizana kuufuatilia.

Mmoja wa waliofuatilia, Christopher Shayo ‘Kimeta', alisema baada ya kumalizika kwa mdahalo huo ameweza kujua pumba ni zipi na mchele ni upi.

"Sijui kama hawa viongozi wa CCM na wajumbe wao wa Bunge la Katiba waliuangalia, lakini kwa kweli wameumbuka mchana kweupe. Upotoshaji wao ulifikia tamati jana," alisema Shayo.

Mfanyabiashara, Festo Minja alisema ufafanuzi uliotolewa na wajumbe wa Tume unapaswa kuwa dira ya majadiliano kwa wajumbe wa Bunge la Katiba lililoanza jana bila maridhiano.

Bukoba

Mchuuzi, Derick Edmund anayeuza bidhaa karibu na Hospitali ya Mkoa wa Kagera alisema amefahamu mambo mengi baada ya kufuatilia mjadala huo.

Alisema hoja zilizotolewa na Jaji Warioba kutetea Rasimu ya Katiba ndizo zilizomvutia zaidi na kusema kwa mvutano uliopo sasa itakuwa vigumu kupata Katiba Mpya hivi karibuni.

Mkazi wa Bukoba, Fadhili Hamis alisema kilichomshangaza wakati wa akifuatilia mjadala huo ni jinsi wajumbe wa Tume walivyotetea msimamo wao bila kutofautiana.

Alisema pamoja na kuwa hapendelei muundo wa serikali tatu, hoja zilizotolewa na wajumbe hao wakati wa mjadala zilionekana kuwa nzito na alivutiwa zaidi na mjumbe wa Tume hiyo kutoka Zanzibar, Awadh Ali Said.

Kigoma

Mkazi wa Masanga, Kigoma mjini, Alphonce Mbasa alisema kwa ufafanuzi uliotolewa juzi, wabunge wakipitisha maoni ya vyama vyao kwa kisingizio cha wingi ndani ya Bunge la Katiba hayatasaidia kwa vile wananchi wanajua nafasi yao.

Mkazi wa Kijiji cha Kalinzi, Kamsige Kamsige alisema wajumbe wa Tume wameonyesha uzalendo na hawakuwa tayari kuyasaliti maoni ya wananchi waliyoyatoa katika kuandaa rasimu zote mbili za Katiba.

Mwanza

Ofisa Taaluma Mwandamizi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Tawi la Mwanza, Charles Kadikilo alisema pamoja na hoja nyingi zinazojadiliwa katika midahalo mbalimbali ukiwamo wa juzi, bado haoni ufumbuzi wa kupata Katiba mpya, bali kinachofanyika ni kila mtu kutetea upande wake.

Alisema inawezekana kila mmoja akawa yuko sahihi kwa upande wake ila kinachotakiwa ni kukaa sehemu moja katika meza ya maridhiano na kuacha tofauti zao za masilahi binafsi na vyama vyao.

Arusha

Kada wa CCM, Lembrise Sirikwa alisema mdahalo wa juzi umemsaidia kujua mambo mengi ambayo yalikuwa yamejificha... "Nimefuatilia kwa makini mjadala, kweli kuna mengi nimejifunza na kama kweli tunataka katiba bora ni muhimu kuzingatia kujadili Rasimu iliyopo bungeni na si vinginevyo."

Fundi wa magari, eneo la Sakina, Godi Kweka alisema kati ya midahalo yote ya Katiba iliyofanyika, amevutiwa na mdahalo wa juzi, kwani ulikuwa ni wa kutoa elimu na kuweka kando ubabaishaji ambao umetawala majadiliano juu ya Bunge la Katiba.

"Nilimpenda sana yule Profesa Kabudi, ametupa historia na elimu juu ya Katiba, kweli alichokisema ni muhimu kukifuata kwani Katiba ni ya wananchi na si ya viongozi," alisema Kweka.

Mkazi mwingine, Julius Nkya alisema mdahalo wa juzi umechelewa kwani ulitakiwa kufanyika mapema kwa kuwa ndiyo umetoa dira ya ambacho kinapaswa kufanyika na ni busara yaliyojadiliwa juzi kufuatwa na wajumbe wa Bunge la Katiba na Serikali.

Iringa

Mfanyabiashara wa Miyomboni, Iringa, Peter Kibona alisema wajumbe wa Tume walitumia fursa hiyo kutoa majibu ya maswali mengi ya msingi kuhusu Katiba Mpya ambayo wanasiasa wanaopingana bungeni hawana majibu yake.

"Sasa tumeelewa kuwa hata kitendo cha kuivunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya kukamilika kwa mchakato wenyewe kilifanywa kimakosa," alisema Kibona na kuongeza:
Kwa msingi huo, Katiba haiwezi kupatikana. Wito wangu kwa viongozi, watumie busara au la Bunge la Katiba lisimamishwe yapatikane maridhiano.

Mfanyabiashara wa kanda za muziki karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Iringa, Lema Raymond alisema alilazimika kuongeza sauti wakati wa mdahalo huo ili kuwezesha wananchi kupata ufahamu juu ya mchakato wa Katiba mpya.

Chanzo:Mwananchi
 
Kuna umuhimu wa ITV kutuwekea online au kurusha tena mdahalo ili tuliokosa nafasi tuweze kupata hiyo elimu.
 
Tumekwisha amini ule usemi wao kuwa wamejaribu na wameweza na sasa wanasonga mbel!!
Na Tanzania kwanza ulaya badae sana kama balali
Wao wanapanga nani wakuchukuwa nchi coz nchi ni yao na watoto wao wengine wakimbizi

Tunakubaliana nao ila muda wakuwauliza nadhani haupo mbali watatafuta pakujibia watakosa
 
nchi zote zilizo endelea daima husisitiza midahalo (dialogue) ili kuruhusu michango kinzani, kwayo kila wazo huchambuliwa kwa kuzingatia umuhimu wake, faida na hasara ukizingatia wakati husika. maswali magumu huulizwa na majibu ya kina hutolewa, wanaopinga hushawishiwa kwa hoja. hoja zote kuheshimiwa, watu hawazomeani, kubezana nk. hawapangwi kushangilia au kuzomea wachangiaji au watoa mada bali uweledi na nguvu ya hoja hutawala. ni imani yangu, kama midahalo ikipewa msukumo unaostahili, tutaweza kama taifa kukabiliana na changamoto nyingi tulizo nazo, katika taasisi za elimu ya juu imekuwa zikifanyika dialogue kwa jina la public lectures japo kuna elements za kisiasa zinajipenyeza kwa maslahi binafsi au ya kikundi/taasisi fulani nchini. It is therefore, wise to conclude that for healthy Tanzania, we all need more dialogues/debates na tuachane na ushabiki usio na msingi.., God Bless us all, God Bless Tanzania!
 
Kuna umuhimu wa ITV kutuwekea online au kurusha tena mdahalo ili tuliokosa nafasi tuweze kupata hiyo elimu.
Napendekeza ITV itumie weekend zote mpaka hawa wanaoshupaa bungeni watakapokuwa wamemaliza huo upuuzi wao huko Dodoma ,nadhani ngoma itakuwa droo wakati wa kupiga kura. Ombi ikikataliwa na wananchi tule kiapo cha kuiadhibu ccm wote watakao kuwa wameshiriki,except Deo,Lembeli,Lugola, na wengine watakaoonyesha uzalendo tuwaingize kwenye safu ya uongozi wa ukawa hapo mwakani. Thanks
 
Ulikuwa ni tone la mambo mazuri tunayoyakosa kutokana na udhaifu wa vyombo vyetu vya habari. Hongera sana ITV kwa walau mara moja kuandaa presenters sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi.
Ndio maana Mzee Butiku aliuliza kuwa wanaounga mkono (hoja moja) wanyooshe mikono/kusimama na akawaambia waandishi wapige hiyo picha ili japo iingie kwenye historia.
 
Ule mwiba lakini wapumbavu siku zote hushupaa bora sisi wajinga. CCM Imefika mwisho wa uongo wake sasa ni ukweli mtupu hongera ITV na Radio One kwa mdahalo mzuri sana.
 
Tuwe wa wazi jamani. Tatizo ni ccm kuona Tanzania ni ya kwao na watanzania wote wako chini yao kiasi kwamba wanaweza kuwafanyia na kuwafanya lolote wakati wowote wasiwe na lolote la kufanya wala mahala pa kulalamika na kudai haki zao. Nasi asiyefahamu hili?


nchi zote zilizo endelea daima husisitiza midahalo (dialogue) ili kuruhusu michango kinzani, kwayo kila wazo huchambuliwa kwa kuzingatia umuhimu wake, faida na hasara ukizingatia wakati husika. maswali magumu huulizwa na majibu ya kina hutolewa, wanaopinga hushawishiwa kwa hoja. hoja zote kuheshimiwa, watu hawazomeani, kubezana nk. hawapangwi kushangilia au kuzomea wachangiaji au watoa mada bali uweledi na nguvu ya hoja hutawala. ni imani yangu, kama midahalo ikipewa msukumo unaostahili, tutaweza kama taifa kukabiliana na changamoto nyingi tulizo nazo, katika taasisi za elimu ya juu imekuwa zikifanyika dialogue kwa jina la public lectures japo kuna elements za kisiasa zinajipenyeza kwa maslahi binafsi au ya kikundi/taasisi fulani nchini. It is therefore, wise to conclude that for healthy Tanzania, we all need more dialogues/debates na tuachane na ushabiki usio na msingi.., God Bless us all, God Bless Tanzania!
 
Wapumbav.u hata sasa shingo zao zimeshupaa na hawataki kuelewa
 
katika kipindi hiki ambapo bunge la katiba limerejea, nashauri serikali IPIGE MARUFUKU midahalo yote ya katiba. ikiruhusiwa ni kama kushusha hadhi ya bunge
 
Kuna haja ya ITV kuweka channel yao katika package za DSTV Maana nahisi nakosa mengi!!
 
Back
Top Bottom