Wananchi Dar wampinga Makonda agizo la kuwasaka wasio na kazi

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Paul-Makonda.jpg

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

WANANCHI mkoani Dar es Salaam wameungana na Meya wa Jjiji hilo kupinga tamko la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, la kuanzisha msako wa nyumba kwa nyumba kuwabaini wasiokuwa na kazi maalum.

RC Makonda alitoa tamko hilo siku chache zilizopita akitaka uanzishwe msako wa nyumba kwa nyumba kuwasaka watu ambao hawana kazi maalum na kuwachukulia hatua.

Soma zaidi hapa=> Wananchi Dar wampinga Makonda agizo la kuwasaka wasio na kazi | Fikra Pevu
 
Hivi huyu Mkuu wa mkoa wa Dar ndo yule yule Makonda aliyempiga Mzee Warioba au kuna Makonda mwingine
Ukiwaza sana kuhusu utata wa matamko yake unapata mashaka sana na jinsi atakavyotawala jiji kwa mafanikio
 
Yeye ajiulize kazi aliipataje kama aliipata kirahisi aje kutukamata.
 
kabla ya kufanya hayo maagizo yake angetembelea makampun ya ujenzi na viwanda atatue matatizo yao kwanza!

kama makampuni ya ujenzi yanaengeza faida kubwa sana ,
lakini hakuna mtanzania mwenye ajira huko zaid ya wahindi na wachina tu!
kama kweli ana nia nzuri azunguke kwenye makampuni ya ujenzi na viwanda aone watanzania wanavyo fanyishwa kazi hata kupewa vitambulisho ni shida !
 
Yaani jina la huyu Kijana kila siku lipo kwenye Magazeti na vyombo mbalimbali vya habari kwa mambo ya kijinga kabisa, tunasubiri atoke tamko la aibu kuu ili aondolewe kwenye nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa
 
Yeye wakati amemaliza chuo alikuwa Dar pia bila kazi yoyote. Sasa ameshasahau......!
 
Hao waliomuunga mkono meya nao hawana kazi, makonda aanzie kuwahesabu wao, wamejileta!
 
Huna uzoefu,kuishi kwa kupiga domo.....hadi kupata uoongozi...alafu lack of xposure ni shidaaa
 
kuna majeshi ya vijana wanamaliza vyuo vikuu hawana ajira angewaita awape ajira kwanza
 
Wote wanaopinga juhudi za Makonda ni mashoga, wavuta shisha, makahaba, wauza unga na wauza pembe! Full stop!!

Jee ni pamoja na wale waliompinga kule kwenye Bunge la katiba kuwa ni "weka mbali na smartphone"? Usiwe unatukana bila kufuata uchunguzi
 
Wote wanaopinga juhudi za Makonda ni mashoga, wavuta shisha, makahaba, wauza unga na wauza pembe! Full stop!!

Endeleen kumsifia tu lkn mnamharibia. Peye ukwel mwambien ukwel kusud aendelee kya kiongozi bora.Binafsi huwa sipendi sana mtu anayenisifia tu, Huwa namwona ni mnafiki tu siku nikianguka ndo wa kwanza kunisema vibaya.
 
Endeleen kumsifia tu lkn mnamharibia. Peye ukwel mwambien ukwel kusud aendelee kya kiongozi bora.Binafsi huwa sipendi sana mtu anayenisifia tu, Huwa namwona ni mnafiki tu siku nikianguka ndo wa kwanza kunisema vibaya.
Kwahiyo kumponda pale anapojaribu kupambana na wahalifu ndo kumsaidia....sawa tumekuelewa mr shallow mind
 
Unajua hii nchi sasa sijui hawa wateule wa mzee magu wananini, jana nilimsikia waziri mkuu akionya wanafunzi wanaoishi kwenye mabweni kutotumia, mshumaa, kupika, na kupasi nguo kwa kutumia pasi ya umeme, sasa nikasema mshuma sawa, kupika pia sawa ila swali wapasi nguo kwa kutumia nini?
 
Back
Top Bottom