Wanamume wenzangu hii haiko poa kabisa....we need to change....

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,896
36,213
Habari za muda huu marafiki ndugu na jamaa....ni matumaini yangu kuwa nyote mu wazima wa afya tele na wale ambao afya zao zina mishkeli...basi muumba awajaalie mupate afya njema ili tuendelee na ujenzi wa taifa letu lililodumaa.....

Leo wapendwa ningependa kujuika nanyi katika kisa kisa kimoja cha kweli kabisa kilichomkuta rafiki yangu lakini naamini kabisa rafiki huyu kwa huu mkasa wake anawakilisha kundi kubwa la wanaume wenzangu wenye tabia kama hiyo.....

Miaka ya hivi karibuni huyu swahiba wangu alikuwa na mgogoro kwenye ndoa yao.....ndoa ambayo imedumu kwa miaka takribani kumi huku wakibahatika kupata watoto wawili.....kiini kikubwa cha mgogoro huo ni tuhuma za shemeji kuwa swahiba wangu amekuwa akitoka njia kuu mara kwa mara.....

Mimi nikiwa kama mtu wa karibu na huyo mume wa mtu nikiri kuwa kwa kweli jamaa anatabia hiyo...hii ni tabia ambayo nimekuwa nikiikemea sana kwa huyu jamaa yangu hadi kufikia wakati mwingine tunagombana kabisa.....Hali hii ilipelekea mpaka akawa anamdharau my wife wake.....shemeji kwa kutambua kuwa mimi ni mtu wa kaaribu na mumewe na pale mtaani hatuishi mbali mbali akawa ananifikishia kesi zao mbali mbali zinazohusu ndoa yao....na mimi kwa kadri ya uwezo nikawa najitahidi sana kuweka mambo sawa......
Naweza nikasema kuwa hadi kufikia miaka zaidi ya kumi ya ndoa nimekuwa msaada mkubwa sana katika kuijenga ndoa yao....

Lakini kwa kosa la hivi karibuni shemeji alikuja kuniambia kwa uchungu sana na kwa machozi kuwa hili hawezi kulisamehe kwani yamemfika shingoni.....
Kutokana na juhudi za kuwasuluhisha kugonga mwamba huku nikisaidiana na v mbalimbali na jamaa kuonekana kutokakujali kana kwamba alikuwa amemchoka mke na sisi tukihangaika kama vile vile sisi ndio wenye mke....hatimaye ikatoka taraka rasmi......yule shemeji ni mtu mwenye kipato chake na ninaweza kusema kuwa anamzidi jamaa kwani anafanya kazi kwenye taasisi kubwa hapa nchini na swahiba wangu akiwa ni dereva kwenye kampuni fulani ya kigeni.....kwa hiyo ile taraka haikumfanya kuyumba kimaisha wala kimsimamo....akawachukua wanawe na kumuachia jamaa vitu vyote ndani na kwenda kupangisha nyumba nzima maeneo ya kijitonyama....

Maisha yaliendelea kama kawaida na hatimaye mwaka ukakatika....kwa kuwa yule hatukuwa na ugomvi naye tukawa tunawasiliana sana maana alinifanya kama mjomba wake wa kimjini mjini.....kwa hiyo aliniheshimu na mimi nilimheshimu sana....

Yule shemeji hatimaye akapata mchumba na yule mchumba akawa tayari kumuoa....na shemeji yangu wa zamani akanipa taarifa hizo nzuri nami nikamtakia kila la kheri katika ndoa yake mpya....

Sasa huyu swahiba wangu baada ya kusikia kuwa mzazi mwenzie amepata mwenza ndio visaa vikaanza...safari za kwenda kwa yule mwanamke kwa kisingizio cha kuwajulia hali watoto zikawa mfululizo....wakati mwingine huwa ananishirikisha na huwa namsindikiza lakini mara nyingi anakwenda mwenyewe...wakati mwingine hata nyakati za usiku......wakati anakutana na yule mchumba mpya wa mkewe wa zamani anaanza kumletea vurugu na kumtukana.....shemeji amekuwa akinilalamikia kutokana na tabia ya huyo jamaa kwani anaweza kamharibia kwa jamaa yake huyu mpya....na ametishia kumpeleka polisi kama akiendelea na tabia hiyo maana amevumilia ameshindwa.....

Nami nimekaa na jamaa kitako na nikamuambia vyakutosha lakini jamaa amegoma kuelewa...nami nimeamua kumuacha yatakayomkuta yamkute.....

NB:nimeileta hapa jukwaani kama funzo kwa wanaume wenzangu....kama umeamua kumuacha mkeo tena kwa taraka tatu basi...huyo tena hayupo kwenye himaya yako....hivyo ni vyema umuache aendelee na maisha yake.....
 
baada ya kumwacha anashikwa wivu kwa mtalaka kupata mume mpya.........wapo baadhi wa wanaume wanakuwa na tabia hiyo akikukuta mahali anakufanyia fujo yote hayo kutokutaka kuona unapata mwingine au kuonekana alikuwa dhaifu kushindwa kuendeleza ndoa yao.
 
Ndio maana nikaileta hapa ili iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama hiyo.....
 
Kweli, tujifunze. Kama umeachana na mtu, tena mkapeana talaka kabisa, ya nini umfatefate? Ni wivu wa kitoto sana..

Ndio maana watu wanaogopa kuoa/kuolewa na single parents, coz hata kama dada wa watu hana time na jamaa, lakini yule jamaa aweza kuwa mwiba kwenye penzi lao.
 
Labda ameanza ku mmiss mkewe hivyo anahisi ameanza kumpenda tena,mshauri warudiane.Unajua wana ndoa huwa hawaachani.
Sidhani kama amemmiss. Hii inaitwa wivu. Sababu jamaa alijua huyo mwanamke atakuwa single maisha yake yote. Sasa roho inamuuma kuona amepata mwanaume mwingine.
 
Kweli, tujifunze. Kama umeachana na mtu, tena mkapeana talaka kabisa, ya nini umfatefate? Ni wivu wa kitoto sana..

Ndio maana watu wanaogopa kuoa/kuolewa na single parents, coz hata kama dada wa watu hana time na jamaa, lakini yule jamaa aweza kuwa mwiba kwenye penzi lao.
Kweli kabisa binamu......yule mwanadada amejitahidi sana kutumia njia za kidiplomasia lakini inashindikana....hebu fikiria anakuja mpaka usiku wa manane na kugonga mlango kwa fujo na akifunguliwa cha maana hana zaidi ya kusema nataka kuwaona wanangu....

Nimejaribu sana na kumuweka chini na kumueleza maana ya upuuzi anaoufanya....lakini yeye hasikii....tena mpaka wakati mwiingine tunagomba akinishutumu kuwa mimi na yule mwanamke letu moja.....

Na kibaya zaidi ni kwamba kila hatua wanayofikia katika mipango yao ya ndoa ananiambia.....na amenitambulisha mpaka kwa huyo mchumba wake mpya....akimuambia kuwa mimi ni mjomba wake kabisa.....kwa hiyo jamaa ananiheshimu na tunaheshimiana sana.....na jamaa ni mstarabu sana.........
 
Mwambie huyo swahiba wako aheshimu maamuzi yake. Kama alikosea ndio imekula kwake. Amuache dada wa watu aendelee na maisha yake.
 
Acheni amrudie mkewe,unajua kuishi na mwanamke miaka kumi unalala nae na kuamka nae inahitaji uvumilivu hivyo yaliomtokea jamaa iwe kamchoka au vyovyote ujue ndio ndoa hiyo.
 
Kama watoto ni wa kubwa wa kulelewa na mt mwngn tofauti na mama yao mwambie bibi dada awapeleke kwa bibi yao wakakae huko hata Mwaka, hafu hilo jimbulikenge liwe linaenda huko kuwaona kwa mama yake, atafute sababu nyingine mana mijianaume mengine ni hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom