Wanamichezo sita wajitokeza kuwania Urais TFF

Wanamichezo sita wajitokeza kuwania Urais TFF

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
WANAMICHEZO sita wamejitokeza kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Agosti 16, mwaka huu jijini Tanga.

Taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Benjamin Kalume imewataja wanamichezo hao kuwa ni Ally Mayay Tembele, Ally Thabit Mbingo, Mbette Mshindo Msolla, Mustapha Salum Himba, Shija Richard Shija na Rais wa sasa Wallace John Karia.

Soma Pia: Ally Mayayi atangaza kugombea Urais TFF

Pia taarifa imesema wanamichezo 19 wamerudisha fomu kuomba Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia kanda mbalimbali.
1750772010271.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom