Wanamgambo wa Al-Shabaab wavamia hoteli Mogadishu, Somalia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Wanamgambo wa Al-Shabaab nchini Somalia wamehusika katika makabiliano ya polisi na vikosi vya usalama katika hoteli moja iliyopo mji mkuu wa Mogadishu.

Kundi la Al-Shabab limekiri kutekeleza shambulizi hilo katika hoteli ya Afrik ambalo lilianza na bomu lililokuwa limetegwa kweye gari Jumapili mchana.

Hadi kufikia sasa, haijafahamika ni watu wangapi waliojeruhiwa lakini shirika la habari la AFP limeripoti kuwa karibu watu watatu wamefariki dunia.

Kundi hilo ambalo linahusishwa na kundi la wanamgambo la Al-Qaeda, mara nyingi hutekeleza mashambulizi dhidi ya serikali.

Inasemekana kuwa gari moja liligonga eneo la mbele la hoteli hiyo na kulipuka kabla ya mshambuliaji aliyekuwa amejihami kwa silaha kuvamia jengo la hoteli, kulingana na maafisa na wengine walioshuhudia shambulizi hilo.

"Mlipuko huo ulifanya hoteli hiyo ikaanza kutetemeka wakati tukiwa ndani tunaendelea na mzungumzo. tulishutuka, tusijue la kufanya," aliyeshuhudia Ahmed Nur amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Maafisa waandamizi wa usalama Mohamed Dahir ameliambia shirika la AFP kuwa raia wawili na afisa mmoja wa usalama wamethibitishwa kufariki dunia, "lakini idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka."

Ambulances are seen near the scene of a car bomb explosion

Magari ya kubeba wagonjwa yameonekana yakiwa karibu na eneo lililoshambuliwa kwa bomu.

Wanamgambo hao waliilenga Hotel Afrik licha ya kwamba ipo kwenye eneo lililo chini ya ulinzi mkali na ipo karibu na uwanja mkubwa wa ndege mjini humo, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC aliyeko Mogadishu, Bella Hassan.

Hoteli hiyo ni maarufu sana nchini humo na mikutano mingi ya maafisa wa serikali ya Somali hufanyika hapo.
Msimamizi wa polisi wa eneo hilo amesema wabunge kadhaa na maafisa waandamizi wa jeshi walikuwa ndani ya hoteli hiyo wakati shambulio hilo linatokea.
Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionesha moshi mkubwa ukifuka katika eneo hilo mapema Jumapili.

Shambulio hilo linatokea ikiwa ni wiki kadhaa tu baada ya aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump kuagiza kuondoka kwa wanajeshi 700 ambao wamekuwa wakiunga mkono vikosi vya usalama vya eneo hilo dhidi ya makundi ya wanamgambo wakiwemo wanamgambo wa Al-Shabab.

Kuna hofu kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani huenda kukaongeza ukosefu wa udhibiti wa matukio kama hayo katika taifa ambalo litafanya uchaguzi mwezi ujao.
 
Pesa kubwa wanayotumia kuwadhibiti wanamgambo kama ingetokea wakaacha mapigano nazani inge boost maendeleo yao kuliko kupigana daily
 
Inasikitisha sana! Wema bado hawajazaliwa kwenye hii dunia.
 
Back
Top Bottom