Wanaharakati wameonyesha njia, tuwaunge mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati wameonyesha njia, tuwaunge mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PETER JOHN MLAY, Feb 28, 2012.

 1. P

  PETER JOHN MLAY Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwapongeza sana na kuwaunga mkono wanaharakati wote waliojitokeza katika kuandamana na kuonyesha hisia zao kali dhidi ya serikali wakati wa mgomo wa madaktari takribani wiki mbili zilizopita sasa.

  Ukombozi wa nchi yetu unahitaji watu kama hawa na kwa pamoja tutaweza kulikomboa taifa letu. Tukumbuke kazi hii ya ukombozi wa taifa sii kazi ya vyama vya siasa pekee yao, wanaharakati wanayo nafasi muhimu sana, tuwaunge mkono sasa.

  Wakati Serikali dhalimu inapo pambana na wanaharakati, vyama vya upinzani na wanamapinduzi wote; ni jukumu letu kuunganisha nguvu zetu ili ukombozi uweze kuja mapema.

  Mapambano lazima yaendelee.
   
 2. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa. Nchi changa km yetu zinazokabiliwa na majanga yanayotokana na ubinafsi wa viongozi, kuporwa rasilimali zake na kuangamia kwa misingi ya utaifa zinahitaji wanaharakati wanaojitoa kuwasilisha hisia za wengi. Hata mataifa makubwa yaliyoendelea, yalipitia harakati kama hizo na zaidi ya hapo. Maendeleo yao ni jitihada au harakati za mababu zao.
   
 3. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  VEN CREMOC !!!!!!!!!!!!!! A lute continua !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Wangapi wako tayari kufanya maandamano kwa ajili ya ukombozi wa kweli wa Taifa letu. Kama ni watu; wako wengi. Lakini wana harakati; WACHACHE.

  Mapambani sio lazima yawe ya mtutu. Hata wananchi wakigoma kwa kukaa kimya kwa wiki nzima ujumbe utawafikia walengwa. Lakini wangapi wako tayari?

  Kama wewe mwananchi mwenzangu uko tayari kwa ukweli basi kuazia kesho vaa ukanda wa blue kwenye mkono wako wa kulia. Tijambulishe kuwa wewe ni mwana harakati wa kutetea taifa la Tanzania na watu wake na rasilimali zake.


  MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE NA RASILIMALI ZAKE.


   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kumbe wanaharakati nao walishiriki katika mazungumzo ya kuleta suluhu baina ya serikali na madaktari? maana nilikuwepo wakati wanakamatwa Pale daraja la Salenda sikumuona Waziri Mkuu (mtoto wa mkulima). Hata hivyo mleta huu uzi hana hoja maana wakati huo alikuwa hajawa mwanachama hapa JF.
   
 5. P

  PETER JOHN MLAY Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushiriki wa wanaharakati katika hili la madaktari haukuwa ni katika vikao kama unavyo jaribu kufikiri hapa, hapana, mchango wa ukombozi unaweza ukawa wa jinsi yeyote ile hata kwa wewe kuandika mada zinazogusa wengine na kuwaamsha katika usingizi wa pono walio lazwa baada ya kupewa dozi za kidumu chama cha majambazi!
   
Loading...