Wanafunzi Wapewa Masharti

Endaku's

JF-Expert Member
May 25, 2007
321
47
Halima Mlacha--Habari leo

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Mlimani (UDSM), Elimu (DUCE) na Mkwawa, waliosimamishwa masomo kutokana na mgomo, wameamriwa kujaza fomu upya za udahili na kulipa asilimia 40 ya ada kabla ya Januari mosi mwakani ndipo warejeshwe vyuoni.

Uongozi wa vyuo hivyo umesema watakaokaidi sera ya kuchangia kwa kulipa asilimia 40 ya ada na kujaza fomu hizo, watahesabiwa wamejifukuzisha. Kiongozi mmoja wa UDSM alisema Dar es Salaam jana kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kulipa ada kuonyesha kukubaliana kwao na sera ya uchangiaji kwa vitendo. A

lisema fomu za udahili zinapatikana katika ofisi za elimu za mikoa na kupitia tovuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM na kwamba kila mwanafunzi atatakiwa kujaza fomu tano. Kiongozi huyo alisema fomu zitumwe kwa Mkurugenzi wa Masomo wa UDSM, Mkuu wa Chuo cha DUCE na Mkuu wa Chuo cha Mkwawa kwa njia ya Posta.

Wanafunzi wa vyuo vikuu saba nchini walirudishwa nyumbani kwa muda usiojulikana kutokana vurugu za kudai sera ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu ifutwe au kufanyiwa marekebisho. Wanafunzi hao walikuwa wanataka wapewe mikopo asilimia 100 badala ya utaratibu wa sasa ambapo wanakopeshwa asilimia 60, 80 na wengine 100 ya ada na gharama nyingine kulingana na uwezo wao wa kujilipia gharama hizo.

Serikali imeunda kamati ya watu saba kupitia sera ya uchangiaji elimu ya juu na kutoa mapendekezo ya uboreshaji. Akizungumza wakati wa kuahirisha Bunge mwezi Oktoba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa asilimia 100 ni kitu kisichowezekana.
 
Last edited:
Back
Top Bottom