Wanafunzi waanzisha vurugu shuleni

Wanafunzi waanzisha vurugu shuleni

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Geita. Vurugu kubwa zimeibuka katika Shule ya Sekondari Geita baada ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutishia kuchoma shule kushinikiza wenzao wanne wanaoshikiliwa na polisi waachiwe.

Polisi Geita inawashikilia wanafunzi wanne wa shule hiyo tangu Alhamisi baada ya kumpiga, kumjeruhi na kutishia kumuua mwenzao wa kidato cha tano.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Isaya Busagwe amesema mwanafunzi huyo alipigwa Jumamosi iliyopita na walimu waligundua tukio hilo baada ya aliyepigwa kuugua na kuomba ruhusa ya kwenda nyumbani kutibiwa.

Jana Ijumaa Oktoba 20, wanafunzi hao waligoma kuingia darsani, badala yake, waliandamana kwenda kituo cha polisi kushinikiza wenzao kuachiwa huru.

Baada ya juhudi zao kugonga mwamba kwa polisi kuendelea kuwashikilia wenzao, wanafunzi hao walirejea shuleni na kuanza kurusha mawe wakitishia kuchoma moto majengo wakishinikiza wajumbe wa bodi waliokua wakiendelea na kikao shuleni hapo kutatua suala hilo.

Leo Jumamosi asubuhi, wanafunzi hao walianzisha vurugu zingine, hali iliyolazimisha jeshi la polisi kuingilia kati na kufanikiwa kuzidhibiti.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita(OCD), Ally Kitumbo aliyeongoza kikosi cha kutuliza ghasia kudhibiti vurugu hizo hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akisema yeye siyo msemaji na kazi yake ni kulinda amani na utulivu.

Katika vurugu hizo mwandishi wa habari hii naye amejikuta akiwekwa chini ya ulinzi na kunyang'anywa simu na askari polisi kabla ya kunusuriwa na OCD na kuruhusiwa kuendelea na kazi.

- Mwananchi
 
Wapigwe tu...hatuna namna nyingine. Migomo ya kuharibu mali za shule hizo ni zama za kale.
 
Hao wanafunzi si wanajua maana ya uhalifu, si waache vyombo vya usalama vifanye kazi yao. Haya mambo ya mob justice ni ya kijinga sana.
 
Polisi wangetengua viuno hata vya wanafunzi watano ingekuwa poa
 
Kama umesoma shule mpaka unamaliza hakujatokea timbwili lolote baina ya waalimu na wanafunzi utakuwa mtu wa ajabu sana
 
Uongozi wa wanafunzi ni dhaifu, na unalea uharifu. Kidato cha 5 huonewa na wa cha 6. Mwanafunzi anapigwa, anaugua mpaka kuomba ruhusa kwenda tibiwa nyumbani ndio kipigo alichopigwa kinagunduliwa na walimu.
 
Hao wachache dawa yao ni ndogo tu.
Unafunga shule then unawatangazia kuwafukuza shule huku wangali majumbani kwao.
Tuliwahi kufanya upuuzi kama huu, tukachoma jengo la staff na gari kubwa ya shule enzi zetu. Mambo ya kitoto sana haya.
 
Huwa kuna spirit Fulani hivi either ya kishujaa au ya kipumbavu kuwa lazima uache history.
Hii huwa inawakost wengi sana. Nakumbuka tukiwa high school uniforms zilichelewa kuna watu walitaka kuanzisha maandamano kisa uniform tu kuchelewa.
Pia kuna kipindi fulani nikiwa chuo kuna lecture alikuwa haeleweki kuna watu wakaandaa petition kila mwanafunzi asaini tumtoe lecturer. Binafsi nilipinga niliona ni ujinga wa aina yake while kuna library na resourse nyingi tuu. Inshort hao watoto wanataka hiyo history yaani watakaokuja wahadithiwe.
 
Back
Top Bottom