MKWEAMINAZI
JF-Expert Member
- May 28, 2023
- 930
- 1,299
Wadau nawasabahi,
Katika hali ya kutisha na kustaajabisha ni kawaida kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jiji la Dar kuwaona usiku wakiwa katika uniforms zao na mabegi yao migongoni wakiwa barabarani na kwenye vituo vya daladala na mabasi ya Mwendokasi wakigombania usafiri.
Nimekuwa najiuliza maswali yafuatayo:
1. Je, tatizo ni muda wa kutoka shuleni ndio mbovu?
2. Je, shule na makwao ni mbali?
3. Kwanini Serikali isiwapangie kwa lazima shule za karibu na maeneo wanayoishi ili wasihangaike na usafiri?
4. Je, ni wazazi ndio wanawahamishia wanafunzi shule za mbali na makazi yao au serikali?
5. Je, daladala na mabasi ya Mwendokasi hayataki kuwachukuwa wanafunzi vituoni ndio maana wanachelewa mpaka huo usiku?
Wakati umefika kwa Waziri mwenye dhamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakishirikiana na Serikali kufanya maamuzi magumu katika hili tatizo, kwani madhara yake ni makubwa sana kwa wanafunzi wetu ukizingatia kuna wanafunzi wa shule za msingi wengi wao umri ni mdogo sana na ubakaji na ulawiti umeshamiri sana katika jiji hili.