BADO MMOJA
JF-Expert Member
- Jul 19, 2012
- 2,195
- 1,346
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Chinangali iliyopo manispaa ya Dodoma wameshindwa kufanya mitihani kwa madai kwamba pesa za elimu bure hazitoshi kutengeneza photocopy mashine ya shule na kwa uelewa wa Mkuu wa Shule hiyo hana njia mbadala ya kufanya maisha ya kitaaluma yaendelee bila kutegemea mashine hiyo.
Swali la kujiuliza hivi mtu hadi kuwa Headmaster kabla ya hizi mashine kuja watu walikuwa hawasomi? Nilichokigundua ni kwamba walimu wana hasira kali ya kukosa kuchangisha ile michango walikuwa wanafaidika nayo kwa hiyo wanaweka vikwazo ili ijulikane kwamba mpango wa elimu bure umekwama.
Sijui kama Mkurugenzi na Afisa Elimu wa Manispaa kama wanalitambua hilo, kwakweli inasikitisha sana ubunifu wa wasomi wetu ni mdogo sana wanazingatia pesa kuliko ukweli hivi walimu wa sasa hawawezi kuandika mitihani kwa mkono mpaka watumie mashine tu? Wakiandika kwa mkono ni nzuri zaidi kuliko kwa mashine kwani sehemu ya somo la uandishi mzuri lakini hapo ni pesa mbele.