Wakristo nchini Kenya wametumia
maadshimisho ya misa za sikukuu ya
pasaka kote nchini humo
kuwaomboleza waathirika wa mauaji
ya wanafunzi wa chuo kikuu cha
Garissa.
Makanisa mengi nchini humo
yaliomba ulinzi wa askari wenye
silaha kuwalinda wakati wa ibada
.Ibada hizo zilikuwa maalumu
kuwaombea marehemu wapatao mia
moja na arobaini na nane waliouawa
na kundi la wanamgambo wa Al
Shabaab ambao waliwalenga
wakristo zaidi katika shambulio hilo.
Wengi wa wanafunzi mia moja na
arobaini na nane waliouawa
walikuwa ni wakristo waliochambuliwa na magaidi wenye silaha wa kundi la Al shabaab.
Katika siku ya kwanza ya
maombolezo ya kitaifa makanisa
mengi yalilindwa na walinzi wenye
silaha.
Askofu wa Kanisa kuu la Garissa
Joseph Alessandro amesema
mashambulizi yametengeneza alama
kwa watu.
"Hali ya wasi wasi na uoga imekuwa
ya kila siku, kwa sababu haya
mashambulizi yamekuja kwa
kushtukiza, hukuwa umejiandaa na
hivyo hali hii inafanya kuwa katika
hali ya wasi wasi muda wote."
Mmoja kati ya waumini
waliohudhuria ibada hiyo anasema
amepata faraja ndani ya kanisa.
"Hakuna mahali popote ambapo ni
salama, lakini hapa kanisani
unaweza kuja na ukampokea Mungu
ambaye anakuwezesha kujifariji
wewe mwenyewe."
Wakati huo huo,vilio na majozi
viliendelea kwa ndugu waliokwenda
kutambua miili ya wapendwa wao
waliouawa katika shambulio hilo la
kigaidi.
Baadhi ya waliofika kutambua miiili
ya ndugu zao wamesema zoezi la
kutambua miiili limekuwa gumu.
"Imetuchukua takribani dakika 20
miili imeharibika ipo nje, imepoteza
maumbo yake hivyo inachukua muda
mrefu kutambua ndugu zetu." walisema
Source: magazetini
maadshimisho ya misa za sikukuu ya
pasaka kote nchini humo
kuwaomboleza waathirika wa mauaji
ya wanafunzi wa chuo kikuu cha
Garissa.
Makanisa mengi nchini humo
yaliomba ulinzi wa askari wenye
silaha kuwalinda wakati wa ibada
.Ibada hizo zilikuwa maalumu
kuwaombea marehemu wapatao mia
moja na arobaini na nane waliouawa
na kundi la wanamgambo wa Al
Shabaab ambao waliwalenga
wakristo zaidi katika shambulio hilo.
Wengi wa wanafunzi mia moja na
arobaini na nane waliouawa
walikuwa ni wakristo waliochambuliwa na magaidi wenye silaha wa kundi la Al shabaab.
Katika siku ya kwanza ya
maombolezo ya kitaifa makanisa
mengi yalilindwa na walinzi wenye
silaha.
Askofu wa Kanisa kuu la Garissa
Joseph Alessandro amesema
mashambulizi yametengeneza alama
kwa watu.
"Hali ya wasi wasi na uoga imekuwa
ya kila siku, kwa sababu haya
mashambulizi yamekuja kwa
kushtukiza, hukuwa umejiandaa na
hivyo hali hii inafanya kuwa katika
hali ya wasi wasi muda wote."
Mmoja kati ya waumini
waliohudhuria ibada hiyo anasema
amepata faraja ndani ya kanisa.
"Hakuna mahali popote ambapo ni
salama, lakini hapa kanisani
unaweza kuja na ukampokea Mungu
ambaye anakuwezesha kujifariji
wewe mwenyewe."
Wakati huo huo,vilio na majozi
viliendelea kwa ndugu waliokwenda
kutambua miili ya wapendwa wao
waliouawa katika shambulio hilo la
kigaidi.
Baadhi ya waliofika kutambua miiili
ya ndugu zao wamesema zoezi la
kutambua miiili limekuwa gumu.
"Imetuchukua takribani dakika 20
miili imeharibika ipo nje, imepoteza
maumbo yake hivyo inachukua muda
mrefu kutambua ndugu zetu." walisema
Source: magazetini