Wanachama wa CHADEMA kama wa Liverpool kocha akiwa mzuri moto wake kama wa kifuu habari ya kufa sahau

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Katika vyama vinavyopata misukosuko CHADEMA inaongoza, huko nyuma tuliona tanu ilivyoangaika kuvimaliza vyama vya upinzani na kuvifanya vife kabisa. Hii ni tofauti na CHADEMA, CHADEMA imejikita mwenye mioyo ya watu ambao wapo serikalini, wapo CCM lakini hawajionyeshi. Mifumo ya chama tawala huko nyuma ilikuwa ya kindugu sana kiasi kwamba waliowahi nafasi wanazifanya miliki yao. Ujio Wa Rais Magufuri angalau umebadilisha sura kwani ameamua kuondoa utawala Wa kindugu kwa teuzi sake, lakini bado anakwama kwani waliokwazika ni wengi.

Kwanini nasema CHADEMA kama Liverpool, ni kwamba CHADEMA haijapata kocha mzuri, aliyepo anababaika sana kwani mbinu zimemuiishia ikiwa CHADEMA ikapata kocha mzuri ikafunguliwa gereza la siasa basi CCM kufutika nusu siku. Ndio maana kauli za Dr. Bashiru zimeelezea uhalisia baada ya kuona CHADEMA wanachama wao vichwa ngumu awabadiriki. Hata CCM inavyoendelea kuwapokea watoro isifurahia sana kwani walipishana na uongozi lakini mioyo yao ipo upande Wa pili kwani malezi yao yamegubikwa na siasa kinzani.
 
Hujatoa suluhisho,kocha sahihi ni yupi ,Hivi mwambe au Sumaye ndo wangekuwa makocha unaona hali ingekuwaje?kocha mkuu wa serikali katika timu yake kuanzia kipa,beki,kiungo,winga a hata washambuliaji kuna ndugu zake.Kwa hiyo undugulisation Tanzania huyu kauchochea mara 10 labda tu bado hujapembua kiyakinifu.

Kiufupi ni kuwa tuna uhaba wa viongozi nchi hii.Hata ukiangalia Viongozi wanaokuwa Daruso huwa kama mazezeta,wapowapo tu baadae wanagombea udiwani huko kwao wanapata.Kwa hiyo tutafute namna ya kupika viongozi vijana ngazi ya vyuo vya kati na vikuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mikedean,
Nilivyolinganisha CHADEMA na Liverpool ni kwamba wapenzi Wa Liverpool hata uwafanyeje awabadiriki kocha atahama atakuja mwingine akiboronga wanakaa kimya akipatia unaweza ukadhani wanatawala dunia. Cdm INA wanachama zaidi ya milioni 15 hawa wote waoga kupambana, kosa la kocha wetu mbowe ni kumleta mshambiliaji aliyekuwa ana nia ya kukomboa tumbo lake sio kukomboa wananchi.

Mshambiaji akaogopa vitisho vya mabeki akastaafu kulinda tumali twake. Kwa sasa wanaoindoka sisi hawatuumizi sana kwani wametofautiana na mwenyekiti, sisi hatutawakata mikia kwani wako wanajazwa mbinu ambazo tutazitumia kusambalatisha chama twawala. Mbowe abadirishe mbinu, apunguze mumkali kwani viongizi wetu kila siku mahakamani inatuchosha sana
 
mgt software,
Wapinzani sasa hivi ni wengi wakupitiliza inawezekana undungu umehama ndani ya CCM lakini unaweza ukawa umehamia sehemu nyingine.

Ni hatari sana ndani ya karne ya 21 tusipo jihadhari na undugu katika uongozi wa aina yeyote ule ni hatari, hatari kweli zaidi ya CORONAVIRUS.

Ni hatari inaleta mawazo mgando na kurudisha taifa nyuma. Kubaini undugu katika chama na ndani ya serikali inawezekana bali kuwaza upendeleo na kuutukuza undugu ni upuuzi na ujinga uliyopitiliza.

Vyama vya siasa ni nchi. Nchi inajengwa na vyama vya siasa, wazalendo, wenye akili, wasio na hisia za u ndugu u ndugu, wenye upendo na taifa lao kama vile alivyotusuka Mwl. Julius Nyerere tukawa kitu kimoja wamoja na taifa moja Tanzania.

Tupingane katika hoja lakini siyo hoja ya kufananisha wapinzani na virusi vya CORONA. Mitazamo hii inajenga nyufa na nyumba ikisha pata nyufa ni rahisi kubomoka. Tuepuke kauli hizi zenye kutu gawa.

Mwisho, tuepuke mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, tunawe mikono na sabuni na maji tiririka kuepuka maambukizi ya corona!
 
Chadema ni kikundi cha matapeli ambacho kimeamua kujihusisha na siasa binafsi niliwadharau sana walipomfukuza Zitto Kabwe kisha wakampokea Lowassa na ndani ya muda mfupi wakamteua kuwa mgombea wa urais.
 
mgt software,
Dr slaa kaondoka Chadema mwaka wa NNE huu lakini kila silu anaadika vitabu juu ya chadema ambayo vinagombewa na kusomwa na wanaccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom