Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,775
- 18,733
Nimekuwa shabiki (sio mwanachama) wa vyama vya Upinzani sana sana Chadema, sio kuwa nawaamini sana watakuwa bora kuliko CCM, no sababu napenda ushindani na ushindani bora utavifanya vyama vyote kuwa bora zaidi kwa sera na usimamizi mzuri, na ndio huleta maendeleo
Sasa Chadema imekuwa ikifanya makosa mengi ya kimkakati ila nitazungumzia ya hivi karibuni ili uzi usiwe mrefu
Kwanza kabisa ni kushiriki uchaguzi mkuu wa 2020, kwa kilichotokea kwenye chaguzi za marudio na uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, ilikuwa ni wazi kabisa kutabiri uchaguzi wa 2020 ungekuwa ni kupoteza fedha tu na kuumizwa bure.
Nikashauri hapa jamvini na kule Twitter Chadema wasishiriki uchaguzi ule, ila nikabezwa na baadhi kunitukana kuniita CCM, ila kilichotoea wote mlikiona
Pili, baada ya uchafuzi ule, ni uchafuzi kweli kama Chadema wanavyoita, Chadema wakapata wabunge na madiwani waliowapata ila wakasema watasusia viti hivyo na kufanya maandamano uchaguzi urudiwe
Nikashauri tena kupitia majukwaa mbalimbali, kuwa kwa kuwa walishaamua kushiriki basi wakubali tu matokeo yale na wachukue wabunge ila iwe somo kwao kuhusu kushiriki hizi chaguzi, suala la kuandamana hadi uchaguzi urudiwe nikashauri ilikuwa ni ndoto za mchana, kwani muitikio wamaandamano wenyewe wanaujua
Lakini nikakejeliwa tena na baadhi yao kutukana, ila kilichotokea kinafahamika, viongozi walikamatwa na CCM wakahonga wabunge wao maarufu wakakisaliti chama
Tatu, ikatokea mwendazake akaenda zake, ikawa kama mwanzo mpya wa matumaini unaanza
Samia akaontesha nia ya kuachana na uhayawani wa Magufuli, alisema atakutana na wapinzani, kitu ambacho jiwe alikuwa hataki hata kukisikia, akafuta kesi kadhaa, akafungulia vyombo vya habari, akina Sabaya, Biswalo Mganga na wengine kwenye ile empire ya kinyama ya Magufuli wakawa wanatolewa
Sasa Chadema wakawa wanatishia Samia akutane nao ama itakuwa ni maandamano na mikutano nchi nzima, na baadhi ya wafungwa aliowaachia kama akina Mdude na Wanaharakati feki kama akina Kigogo (kabla hajawageuka) wakawa wanamtukana Samia
Watu wengi tu waliokuwa hawapendezwi na utawala wa Magufuli nikiwapo mimi, na nikaona kwa watu wengine kama Jenerali Ulimwengu tukashauri Chadema wampe muda Samia na ikibidi wampongeze kumtia moyo kwa anayofanya kwani ndani ya CCM wengi hawapendi mabadiliko hayo na wanataka ule uhayawani wa Magufuli uendelee, sababu unawapa urahisi
Kama kawaida ya wanachadema wengi huwa hawana uvumilivu wa mawazo tofauti wananikejeli plus matusi na kuniita CCM
Sasa kilichotokea kwa sababu ya vile vitisho na matusi kwa Samja ni Mbowe kukamatwa na kupewa kesi ile, yaani Samia aliamua kufuata ushauri wa hilo genge la Magufuli baada ya kuwa frustrated na Chadema
Sasa watu waliokua wakitishia maandamano nchi nzima hawakuweza hata kuandamana kiongozi wao mkuu alipokamatwa kwa mashitaka feki kama yale? wataweza kuandamna kwenye nini?
Hii inatoa picha Chadema hawana nguvu hiyo wanayojiona wanayo, na wana kazi kubwa sana ya kujenga chama chao, kujenga loyalty na dedication kwa wanachama wao, wajitahidi kuepuka confrotation zisizo na ulazima kwa sasa
Nne, Kuhusu kushiriki kwenye mkutano wa TCD
Mwanzoni walipo sema hawatashiriki walikutoa sababu kuwa ni mwenyekiti wao kashikiliwa kwa makosa ya uwongo, baada ya mwenyekiti kuachiuwa ndio watashiriki, hapa niliwaunga mkono walikuwa na hoja ya msingi, lakini mara hii baada ya mwenyekiti wao kutoka wanasema hawatashiriki na kutoa sababu nyingine tena kuwa serikali haijatubu, wanataka serikali ikiri na kutubu makosa ndio ishiriki, kweli?😂😂
Mbowe anasema amesamehe, hana kinyongo na ndi maana alienda kuonana Samia siku ileile alivyotka jela, Samia alikuwa amemuomba msamaha? contradiction
Ila ukimsikiliza Mbowe tena huyo huyo anasema kwa sasa hakuna trust na inabidi wakutane ili kujenga trust taratibu, lakini anasusia huu mkutano wa kwanza na kuukejeli, sasa kwa gesture hii kweli, sasa hiyo trust itaanzaje kujengwa? Mwishowe hata hicho kidogo ambacho wangepata watakosa kabisa.
Chadema wanajidanganya, hawajajifanyia analysis kujua nguvu na udhaifu wao, wanajidanganya wana nguvu nyingi, lakini hawana, hawana leverage ya kuwapa kiburi hicho. Wanasema wana wanachama sijui milioni 6 nchi nzima, sijui mara ya mwisho kufanya hiyo revision ni lini kuhusu uhai wa hao wanachama
Kwenye hii kampeni yao ya Join the Chain ambayo hata mimi nimewachangia sababu nina nia njema nao, wameshindwa kufikisha target yao ya watu milioni 1, yaani watu milioni 1 wangechanga 1000 wangefukisha shilingi bilioni moja kwa sasa, lakini mara ya mwisho kucheki walikuwa hawajafikisha hata milioni 200, sasa hawa wana nguvu gani? hao wanachama milioni 6 wapo wapi?
Chadema ingeajifanyia analysis upya, na pia ingeachana na kudhani kila mtu anayetofautiana nao au kuwa challenge ni CCM au adui yao, ni attitude ya ki dikteta na itawaletea udumavu