DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Zaidi ya wanachama elfu mbili wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Kizota jijini Dodoma wameandama kwa mabango kupaza sauti zao wakipinga matokeo ya kura za maoni za nafasi ya udiwani yaliyotangazwa huku wakidai kuwa zoezi hilo lilikuwa sio la wazi ambapo wameiomba Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Dodoma mjini kuingilia kati ili haki iweze kutendeka.
Katika matokeo hayo aliyekuwa diwani wa kata hiyo Bwana Jamal Ngaluia alitangazwa kuongoza katika kura za maoni kwa kupata kura 216, akifuatiwa na Bwana Rashid Sultan aliyepata kura 105, Sayuni Mwakatika kura 6 na Edwin Balongo akipata kura 4.
Chanzo: ITV