Mwenyekiti wa Kijiji cha Marasomoche Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara aitwaye CHRISTOPHER MWITA 0784902994 maarufu Kama "Getwe" Mwishoni mwa Mwezi Novemba 25/11/2013 Saa 4:00 Usiku, yeye na Wenzake PETER MARWA MAKANDA na MARWA KEMBAKI Walikamatwa na Wanakijiji Wa Kijiji hicho Waliokuwa Wameandaa Mtego wa Kuwanasa Dhidi ya hizo Hila zao chafu baada ya Kupata taarifa Kutoka Kwa Raia Mwema Mmojawapo (Jina limehifadhiwa) aliyeugundua Mpango huo wa Wizi. Licha ya Diwani wa Kata ya Nyansurura MH. JACKSON MWITA 0759490298 (Chadema) Kutoa agizo Kwa Wanakijiji hao Kukaimisha Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Katibu wa Tarafa ya Ikorongo aliingilia Kati Kwa Mgongo wa CCM na Kuwahadaa Wanakijiji hao wa Marasomoche Kuwa hawana Haki/Mamlaka ya Kumwondoa Madarakani Isipokuwa Mkuu wa Wilaya pekee. Kwa Habari za Uhakika toka Kijijini humo zinasema, baada ya Wazee wa Mila wa Kijiji hicho Kuona Uhuni huo Wa Serikali, Waliamua Kuitisha Mkutano wa Kijiji Kizima na Kutoa tamko lenye Maazimio ya Kuwatenga. Star tv Habari