Wanachama na Wafuasi wa Chadema Wananyanyaswa na Kuteswa Vibaya Kata ya Ushirika huko Geita:

Kamanda Francis

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
834
140
Kwa Habari za Uhakika toka Kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Ushirika Wilaya ya Mbogwe Mkoa Mpya wa Geita Bw. DEOGRATIUS PHILIPO SHAYO 0757416254/0688416254 Zinasema Wafuasi.

Wakereketwa na Wanachama wa Chama chake anachokiongoza (Chadema) Wanateswa na Kunyanyaswa Vibaya sana na Jeshi la Polisi Kwa Kushirikiana na Uongozi wa Serikali za Vijiji husika na Diwani wa Kata hiyo ya Ushirika (CCM) Bw. DAUDI SIMON MABENGA Wilaya ya Mbogwe huko Geita.

Bw. Deogratius amesema "Uongozi wa Kata hiyo Umeanzisha Mifumo Mibovu ya Kinyonyaji Kwa Kuwachangisha Ovyo Wananchi Michango Isiyokuwa ya lazima ndani ya Kata hiyo na pale anapotokea Mtu anayehoji Uhalali wa Michango hiyo Jambo la Kwanza anaulizwa Chama Chake na Inapotokea tu Kwamba yeye ni Mfuasi au Mwanachama wa Chadema basi hukamatwa na Kupewa adhabu Kali na Mgambo wa Kata Kwa Amri ya Diwani huyo wa CCM Kabla ya Kupelekwa Polisi ambapo hukutana na adhabu zingine za Mateso" alisema Bw. Deogratius.

Kiongozi huyo wa Chama ameomba Msaada na Nguvu ya Kutosha. ITV Habari
 
Teh teh, wafuasi wa ccm wamezoea dhuluma, ndo maana wanashangaa wafuasi wa chadema kuhoji na kupinga hizo dhuluma! Wananchi wa kata hiyo watumie haki yao ya kikatiba mwaka 2015 kumtoa diwani huyo madarakani. Pia ningeomba uongozi wa chadema kanda, taifa uende katani hapo ili kujionea hali halis!
 
Chadema Bado ni Baba lao! Zaidi 2nauomba Uongozi wa CHADEMA (W) ya Mbogwe Watoe Ushirikiano wa Dhati na Mwenyekiti huyo!
 
CCM wamekosa hoja, wamekataliwa na watu, kilichobaki ambacho wanaweza kufanya ni ugaidi tu

CCM - CHAMA CHA MISUKULE
 
Hizi habari nina wasiwasi ni za kizushi, na za kupikwa. Wewe si ndio umesema mwenyekiti wa tawi (ccm) kaiba mifuko miwili ya cement. Mdogo wangu nakushauri uache udaku.
 
Hizi habari nina wasiwasi ni za kizushi, na za kupikwa. Wewe si ndio umesema mwenyekiti wa tawi (ccm) kaiba mifuko miwili ya cement. Mdogo wangu nakushauri uache udaku.

Tafuta kazi ya kufanya, umri wako bado mdogo ni kwa nini ujidharirishe kutumiwa kukesha JF kwa maslahi ys watu?

Nimekueleza hili kutoka moyoni kama mdogo wangu. Mama yako atafarijika sana siku ukimwambia umeanzisha biashara fulani au kampuni fulani nzuri imekuajiri.

Hii kazi unayoifanya sasa hujitendei haki na elimu uliyoipata imekuwa useless.
 
ChaDeMa hamuishi kulalamikalalamika kila kitu mnataka muonekane mnaonewa tu.mnakera mjue.
 
mazingira ya uonevu kwa wanavijiji ni jadi ya CCM hata kwa wanaccm wenyewe. Uonevu huu umekithili Dodoma hasa wilaya ya Chamwino. Maweo wanashindana kununua magari na pikipiki kwa kutumia njia hizi haramu
 
Hizi habari nina wasiwasi ni za kizushi, na za kupikwa. Wewe si ndio umesema mwenyekiti wa tawi (ccm) kaiba mifuko miwili ya cement. Mdogo wangu nakushauri uache udaku.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Marasomoche Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara aitwaye CHRISTOPHER MWITA 0784902994 maarufu Kama "Getwe" Mwishoni mwa Mwezi Novemba 25/11/2013 Saa 4:00 Usiku, yeye na Wenzake PETER MARWA MAKANDA na MARWA KEMBAKI Walikamatwa na Wanakijiji Wa Kijiji hicho Waliokuwa Wameandaa Mtego wa Kuwanasa Dhidi ya hizo Hila zao chafu baada ya Kupata taarifa Kutoka Kwa Raia Mwema Mmojawapo (Jina limehifadhiwa) aliyeugundua Mpango huo wa Wizi. Licha ya Diwani wa Kata ya Nyansurura MH. JACKSON MWITA 0759490298 (Chadema) Kutoa agizo Kwa Wanakijiji hao Kukaimisha Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Katibu wa Tarafa ya Ikorongo aliingilia Kati Kwa Mgongo wa CCM na Kuwahadaa Wanakijiji hao wa Marasomoche Kuwa hawana Haki/Mamlaka ya Kumwondoa Madarakani Isipokuwa Mkuu wa Wilaya pekee. Kwa Habari za Uhakika toka Kijijini humo zinasema, baada ya Wazee wa Mila wa Kijiji hicho Kuona Uhuni huo Wa Serikali, Waliamua Kuitisha Mkutano wa Kijiji Kizima na Kutoa tamko lenye Maazimio ya Kuwatenga. Star tv Habari

Naona umehamua Kubishana hadi na TV.
 
Tafuta kazi ya kufanya, umri wako bado mdogo ni kwa nini ujidharirishe kutumiwa kukesha JF kwa maslahi ys watu?

Nimekueleza hili kutoka moyoni kama mdogo wangu. Mama yako atafarijika sana siku ukimwambia umeanzisha biashara fulani au kampuni fulani nzuri imekuajiri.

Hii kazi unayoifanya sasa hujitendei haki na elimu uliyoipata imekuwa useless.

Katika elfu saba per day apatayo akimpelekea mama yake elfu mbili kwake ni mafanikio. Ndio shida ya akili zilizo dumaa, hao anaokesha kuwa tetea hata uwepo wake hawautambui.
View attachment 126806
 
Hizi habari nina wasiwasi ni za kizushi, na za kupikwa. Wewe si ndio umesema mwenyekiti wa tawi (ccm) kaiba mifuko miwili ya cement. Mdogo wangu nakushauri uache udaku.

TANGAZO! TANGAZO! Used Condom Kama hizi Weka mbali na Watoto...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom