GE2025 Wanachama CCM Minera, Ulanga watishia kurudisha kadi za Chama

GE2025 Wanachama CCM Minera, Ulanga watishia kurudisha kadi za Chama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)zaidi ya 50 Kutokana Kata ya Minepa Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro, wametishia kurudisha kadi endapo jina la Mtia nia Udiwani aliyeingoza kwenye kura za maoni alitorudishwa.

Wakizungumza wakiwa katika ofisi ya CCM Mkoa Morogoro, Wanachama hao wamesema wameamua kusafiri kutoka katika Kata hiyo hadi Ofisini hapo ili kupata majibu kwanini Mtia nia aliyeshinda hajapewa barua ya utambulisho badala yake amepewa mshindi wa nafasi ya pili.

Kwa upande wake Mtia nia aliyeshinda nafasi ya kwanza kura za maoni Bw. Marugu Manosu anasema alipofatilia katika ngazi mbalimbali za Chama amejibiwa kuwa bado jambo linafanyiwa kazi lakini hajui hadi lini.

 
CCM haitegemei wanachama, inategemea familia za Viongozi tu
 
Shetani hana rafiki. CCM kwa sasa ni chama shetani, hakina habari na maamuzi ya wananchi.
 
sasa kuna haja gani ya kusumbua wajumbe kupoteza muda kupiga kura!
 
Kama ndani ya chama wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe uhuni bila kuficha, kipi chakushangaza kama wanawafutia majina chadema kwenye uchaguzi nakuwafungulia kesi zakuwazushia nakubambikiza yaan fusiemu kumejaa mashetani tu na watu wanaoangalia matumbo yao tu

#siasambovuzabongo
#tanzaniaAmka
#backbenchers
 
Back
Top Bottom