Wanachadema, kuondoka kwa Medeye na J. Mwapachu kunatoa funzo gani?

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Gia ya angani ilipofanyika mlimpoteza mpambanaji na askari ambaye pengo lake hadi leo halijapata tiba (kizibo). Huyu si mwingine bali ni Dr. Slaa. Mengi yalisemwa juu ya kuondoka kwa Dr huyu msafi, muadilifu na mwenye haki na aliyekuwa na uchungu wa kweli kwa taifa hili. Lkn wasemaji na viongozi wa juu wa chama walitoa majibu mepesi ya kuwatuliza wafuasi wa chama kuwa ujio wa Lowassa una faida mara tatu zaidi. Atakuja na watu zaidi, na kwa kuwa siasa ni watu basi chama kitafanya siasa zaidi na kukua zaidi.

Lowassa aliingia CHADEMA kwa ahadi za kutia moyo kuwa ana watu wengi na wabunge wengi wa CCM nyuma yake. Lkn wabunge wa CCM hawakufika hata 5. Nawakumbuka Makongoro Mahanga na Ole Medeye (baada ya kukatwa CCM). Na wenyeviti 3 wa CCM, John Gininita, Mgana Msindai na John Mgeja. Nyepesi nyepesi zinadokeza kuwa hawa walikuwa tayari kurudi CCM, lkn kuna ule mchakato ulioanzishwa na JK pamoja na Kinana wa kuwachambua na kuwachekecha wanaotaka kurudi CCM ndiyo umewakwamisha/kuwachelewesha kujitangaza /kutangazwa.

Tangu gia kubadilika angani wabunge wa CHADEMA waliotorokea CCM ninaowakumbuka ni pamoja na : viti maalumu Christowaja Mtinda na (somebody) Mashishanga.

Hivi karibuni tulishuhudia J Mwapachu akilia kwa machungu na kujutia maamuzi yake ya kuihama CCM na kuingia CHADEMA. Akaomba radhi na kutubu kweli kweli.

Babu Duni alirejea CUF na kuwaambia watanzania kuwa ndani ya CHADEMA kila mtu ni kambale.

Leo hii Ole Medeye amehamia UDP na kuwaambia watanzania kuwa hajaiona demokrsia ndani ya CHADEMA kama ilivyokuwa ndani ya CCM.

CHADEMA sasa kaeni chini mjiulize
1. Kuondoka kwa hao wote nini tatizo? Msitoe majibu rahisi kuwa ni haki yao ya kikatiba. Wala msiwape majina kuwa ni wachumia tumbo ama wasaliti. Tuambieni ama mjitafakari kuna nn ndani ya chama?

2. Hii demokrasia inayolalamikiwa na babu Duni pamoja na Ole Medeye kwann haipo?

Hata Mushumbusi ana uzi wake humu anasema CHADEMA imejengwa kwa misingi ya unafiki na hofu. Siyo demokrasia. Hakuna uhuru wa mawazo na maamuzi. Ni kweli haya?

Mnajifunza nn kuondoka kwa Medeye na J mwapachu walioingia kwa gia ya angani?

Nawasilisha.
 
Hawa wanachama walikuwa wanachama kadi tu Na sijui ni lini Mwapachu alichukua kadi ya CHADEMA Na sijui ni lini alirudisha kadi ole inabidi ujiulize ni lini alijiunga CHADEMA na kuondoka CHADEMA utajua kaja CHADEMA bila cheo ameondoka bila cheo ndio utajua umakini wa CHADEMA
 
Ufipa kinachowatafuna had sasa na wanajuta ni kubadili gia angani kwa gafla, Mimi cna iman nao hata kidogo . charity begin at home.
 
Gia ya angani ilipofanyika mlimpoteza mpambanaji na askari ambaye pengo lake hadi leo halijapata tiba (kizibo). Huyu si mwingine bali ni Dr. Slaa. Mengi yalisemwa juu ya kuondoka kwa Dr huyu msafi, muadilifu na mwenye haki na aliyekuwa na uchungu wa kweli kwa taifa hili. Lkn wasemaji na viongozi wa juu wa chama walitoa majibu mepesi ya kuwatuliza wafuasi wa chama kuwa ujio wa Lowassa una faida mara tatu zaidi. Atakuja na watu zaidi, na kwa kuwa siasa ni watu basi chama kitafanya siasa zaidi na kukua zaidi.

Lowassa aliingia chadema kwa ahadi za kutia moyo kuwa ana watu wengi na wabunge wengi wa ccm nyuma yake. Lkn wabunge wa ccm hawakufika hata 5. Nawakumbuka Makongoro Mahanga na Ole Medeye (baada ya kukatwa ccm). Na wenyeviti 3 wa ccm, John Gininita, Mgana Msindai na John Mgeja. Nyepesi nyepesi zinadokeza kuwa hawa walikuwa tayari kurudi ccm, lkn kuna ule mchakato ulioanzishwa na JK pamoja na Kinana wa kuwachambua na kuwachekecha wanaotaka kurudi ccm ndiyo umewakwamisha/kuwachelewesha kujitangaza /kutangazwa.

Tangu gia kubadilika angani wabunge wa chadema waliotorokea ccm ninao wakumbuka ni pqmoja na : viti maalumu Christowaja Mtinda na (somebody) Mashishanga.

Hivi karibuni tulishuhudia J Mwapachu akilia kwa machungu na kujutia maamuzi yake ya kuihama ccm na kuingia chadema. Akaomba radhi na kutubu kweli kweli.

Babu Duni alirejea CUF na kuwaambia watanzania kuwa ndani ya chadema kila mtu ni kambale.

Leo hii Ole Medeye amehamia UDP na kuwaambia watanzania kuwa hajaiona demokrsia ndani ya chadema kama ilivyokuwa ndani ya ccm.

Chadema sasa kaeni chini mjiulize
1. Kuondoka kwa hao wote nini tatizo? Msitoe majibu rahisi kuwa ni haki yao ya kikatiba. Wala msiwape majina kuwa ni wachumia tumbo ama wasaliti. Tuambieni ama mjitafakari kuna nn ndani ya chama?

2. Hii demokrasia inayolalamikiwa na babu Duni pamoja na Ole Medeye kwann haipo?

Hata Mushumbusi ana uzi wake humu anasema chadema imejengwa kwa misingi ya unafiki na hofu. Siyo demokrasia. Hakuna uhuru wa mawazo na maamuzi. Ni kweli haya?

Mnajifunza nn kuondoka kwa Medeye na J mwapachu walioingia kwa gia ya angani?

Nawasilisha.
Kuwa CHADEMA demokrasia inazidi kukua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom