TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
CCM kama chama tawala kilichokaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hakijafanya makubwa sana kwa nchi hii kiasi cha sisi Wananchi kujivunia.
Chini ya utawala CCM maendeleo katika nchi hii yamekuwa ni ya taratibu mno kama mwendo wa konokono.Inashangaza kuona baadhi ya nchi zilizotoka matatizoni kama Rwanda na Angola tayari zinafanya vizuri kiuchumi kuliko sisi tulioishi kwenye amani tangu uhuru.
Naam Watanzania tumekubali sasa kuwa CCM hawana jipya tena,Tumeweka akili na mawazo yetu kwa Chama mbadala ambacho ni CHADEMA.CHADEMA wanasema kwamba CCM ndiyo chanzo cha madhila yanayowakabili Wananchi,Kiasi fulani ni kweli na kwa kiasi fulani Wananchi pia tunastahili lawama.
Ninachowasihi Watanzania tuanze kuwapima CHADEMA kwenye mambo kama haya;Kujenga jengo la Makao makuu lenye hadhi inayoendana na jina la Chama pamoja na namna watakavyokuwa wanaendesha shughuli za Chama chao kisayansi na kitaalaamu zaidi ili kuonyesha matumaini kwa Watanzania ni aina gani ya mabadiliko watayaleta wakipewa madaraka ya kuongoza nchi.