habari ya hapa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 12,791
- 8,748
Habari zenu mabibi na mabwana, ni imani yangu kuwa mu wazima kiroho na kimwili
Nimetembelewa na rafiki yangu yapata wiki moja na zaidi, akitokea Mereran Arusha, urafiki wetu umekuwa ni undugu sasa, tumejiwekea tabia ya kutembeleana kila mmoja anapopata wasaa.
Rafiki yangu yupo katika kipindi cha mpito kwenye mahusiano yake, tangu aje nimekuwa na kibarua kizito cha kumfariji ili awe katika mazingira mazuri, japo sijafanikiwa mpaka sasa, muda mwingi ni MTU mwenye mawazo, amekuwa ni mwenye machozi kila wakati hata chakula hali vizuri hadi mpigiane makelele.
Anamapenzi ya kweli na mtu wake na wapo kwenye mahusiano yapata miaka mitano sasa lakini huyo mwenzie tayari alikuwa na familia sasa huyo shemeji sijui kapata mwingine au ameamua tu kubaki njia kuu? Mimi na weye hatujui, basi kwa rafiki yangu ni tafarani, anahuzunika sana, kingine rafiki yangu alimuazima pesa huyo mpenzi wake 3.8 milion na hataki kuzirudisha kwa madai kuwa kile alichoplan kukifanya kilikwama, kwa kweli rafiki yangu anapata shida sana.
Huyu mtu analia muda mwingi, presha inapanda kila wakati, nimsaidieje maana nimefika mwisho wa akili zangu, nina mgonjwa KCMC natakiwa kusafiri kama siku kadhaa hivi, nitamuachaje na hali yake hii?