Wana jf siowa kufundiswa chama gani................

Wana jf siowa kufundiswa chama gani................

GreatApe

Member
Joined
Sep 20, 2013
Posts
48
Reaction score
6
Napenda kutoa mawazo yangu ya kawaida tu kuhusu chama boara Tanzania kwasasa kwamba;

  • Wana-Jamii Forum sio wanachama wa kufundishwa chama gani ni bora zaidi ya vingine, kwani wanao uwezo wa kutafuta taarifa za nini maana ya chama na siasa. Wananchi ambao hawapati taarifa za vyama na taarifa za kisiasa (hasa wa pembezoni vijijini na wasiokuwa na elimu ya kusoma) ndio wanaohitaji kufundishwa na kuamriwa ni chama gani bora zaidi ya vingine;
  • CHADEMA bila shaka wanaonesha uhalisia wa "People's Power" [kwa rejea nzuri ya mfano soma "Black Panther Party" in Califorinia ndo utapata picha halisi ya maana ya "People's Power"] lakini wasiwasi wangu falsafa hii imewapita wengi hata walioenda shule kiasi kwamba siasa imekuwa ndio muongozo wa kutenda kila jambo Tanzania hata kama halihitaji siasa;
  • Watu wanatumia ushabiki kwa nafasi ya CHADEMA kama anguko la kisiasa lakini inawezekana katika tasnia na maandhari ya siasa ikawa CHADEMA ndo mfano pekeee wa mabadiliko ya kweli, kwani Zito na Dkt. Kitila bado ni wanachama na wanasifa bado, (japo zimepungua mpaka) mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo; wamekomaa hawawezi zira chama kwa uwajibikaji wao;
  • IMANI na MATUMAINI yangu kwa CHADEMA bado ni asilimia 200 (200%) na toaka maamuzi ya Kamati Kuu asilimia ya UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI inapanda kwa kasi kubwa sana.
CHADEMA TUNARUDI NCHINI KUJENGA CHAMA NA NCHI MSIOGOPE KUTUMIA ANY "DISCIPLINE OF POLITICAL CULTURE" KUJENGA CHAMA-HAKUNA UADUI KATI YA ZITTO/KITILA NA KAMATI KUU BALI KUNA UADUI KATI YA WABAYA (............) NA CHADEMA!!!!!!!

"Politics is the holistic way of changing the way of people's life"
 
Back
Top Bottom