Wana CCM tujiulize,hii mbinu inatufaa? Tulitarajia baada ya kuwapeleka magerezani na mahakamani,wapinzani waende wakilia,mbona jamaa wanacheka tu?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,660
Hizi Mahakama za siku hizi zikoje? au watu wamekuwa sugu? mbona tulitarajia wapinzani wakipelekwa mahakamani walau tuone dalili za wao kuwa na stress ,au hata ndugu zao wakilia,

Naona watu hawa wanacheka tu, hawaogopi hata kifungo kinachohusika na tuhuma zao,

Haya magereza yanageuka kuwa yale ya Paulo na Silla ambayo yalikuwa chanzo cha ukombozi wetu? Maana ya enzi ya Nyerere ukipelekwa kweli unajaa tafakuri mpaka unakonda,mapinzani yanatoka na afya zao

Je huu moto ulioko gerezani hauunguzi ? nani anaupoza moto huu katika tanuru walilotupwa shadraka meshaki na abedinego? Maana kwa huku nje moto huu ni mkali kiasi kwamba hata kusogelea tanuru unakufa,mbona waliotupwa kwenye moto huu wanaongea kwa furaha? Nani anaupoza moto huu? Nyie wapinzani mna nini?

Si mko kwenye shimo la simba? tena wana njaa? sasa mbona hawawatafuni ? Nani kawalisha hawa simba bila sisi kujua wakati ni sisi tumewalaza njaa kwa wiki ili wakiwaona wawararue?

Naomba majibu
Kidumu chama cha mapinduzi!
 
Lumumba wao wenyewe hawaelewani. Hivi washaujibu waraka wa wazee?

Ndiyo maana hata kesi zao za kubumba dhidi ya wapinzani hazina vitisho
 
Back
Top Bottom