WAUMINI 13 wa dini ya Kiislamu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Arusha kwa kosa la shambulio la kudhuru pamoja na kuvuruga ibada.
Watuhumiwa hao walifikishwa Mahakamani hapo mbele ya Hakimu James Karanyemaha na walisomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali Innocent Njau.
Njau alidai kuwa Aprili 13, mwaka huu, majira ya saa 1 usiku, washitakiwa hao walivamia katika Msikiti wa Masjid Taqwa uliopo maeneo ya Sanawari katika Manispaa ya Arusha na kumshambulia Imamu wa msikiti huo na kumdhuru.
Ilidaiwa kuwa mara na baada ya kumshambulia walimtoa Imamu huyo kwa nguvu nje ya msikiti huo na kusababisha kuvunjika kwa ibada iliyokuwa ikiendela mahali hapo.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa hao wote kwa pamoja walimshambulia kwa kipigo na kumsababishia maumivu makali katika mwili wake.
Pia ilidaiwa kuwa wakati wanafanya vurugu hizo Msikitini hapo na kumshambulia, washitakiwa hao walimnyanganya Imamu huyo kipaza sauti na kwenda katika msikiti mwingine kufanya fujo.
Washitakiwa hao ni Hamisi Omari Mlangida, Abbas Omari, Hassan Omari, Waziri Omari, Omari Munga, Hamad Omari Saitoti, Hamis Omari Mollel, Ramadhani Omari Mollel, Haassan Juma, Abraham Jumanne, Abbas Hussein Masoud, Hassam Abubakari na Haruna Abeid.
Washitakiwa wote walikana mashitaka na wako nje kwa dhamana kwa kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja kila moja mwenye uwezo wa kusaini Sh laki nane kila mmoja.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi hapo Aprili 28, mwaka huu, itakapotajwa tena Mahakamani hapo.
Source: Nifahamishe.com