GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,216
Nyie WAMILIKI wa hizi Hotel au Baa hasa za hapa mjini kwani mna AGENDA gani na sisi Wateja wenu?
Mnajua kabisa kuwa mnatuuzia wenyewe Pombe na Mivyakula yenu ambayo sometimes ni Viporo au mchanganyo wa Kiporo na Fresh halafu milango ya MSALANI ( Chooni ) mnaifunga tena kwa KUFULI.
Sasa ni bora basi hii milango muifunge na funguo labda ziachwe hapo hapo tu jirani na huo mlango lakini cha KUUDHI na KUKERA utakuta funguo wa huko Chooni upo Kaunta hivyo ukishikwa na HAJA basi inakulazimu kwanza uwavuke Wateja wote pale Hotelini / Baa kisha uombe funguo huku kila Mtu " akikukodolea " mimacho na akijua kabisa kuwa unaenda Msalani.
Kwanini mnafufanyia hivi lakini? Ina maana mnatukomoa au mnataka tu kutuchoresha? Kuna " mijitu " mingine inakuja humo Hotelini / Baa kutafuta tu UMBEA sasa unaweza " mnyamwezi " ukashikwa na haja ya kushusha " Gogo " halafu hapo hapo hao Wambea wapo na watakachokifanya ni kutegesha tu Saa zao utadhani Refarii wa Mpira Chang'walu huku wakihesabu dakika ambazo unakaa Chooni na ikitokea ukakaa huko dakika 20 au 30 nakuambia muda utakaorudi tu hapo Kitini Wewe ndiyo utakuwa " Breaking News " ya Wateja hapo huku wakikudhihaki kwa maneno kibao.
Ombi langu kwenu wamiliki wa Hoteli au Baa hebu hizo FUNGUO za hayo maeneo yenu hakikisheni mnaziweka tu jirani na mahala husika pa tukio kwani kuna siku nyingine hii tabia ya kuweka funguo KAUNTA mtajikuta Mtu anaufuta hapo funguo huku akiwa tayari keshamaliza Kazi " Surualini " na mkimpa huo funguo huko chooni anaenda tu kama geresha kama si kunawa na tambueni kuwa Binadamu tunatofautiana kwani kuna wengine wana aibu na hawawezi kutembea hadi huko ulipo funguo hivyo ukawa ni usumbufu mkubwa kwao / kwetu.
Tusaidieni katika hili tafadhali na tutashukuru kwa ushirikiano wenu.