Wameweka taa za kuongozea magari lakini za waenda kwa miguu mwakani

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Yaani haya ni maajabu, katika jiji la Mwanza barabara iendayo Musoma eneo la Buzuruga zimewekwa taa za kuongozea magari lakini hazikuwekwa taa za kuongoza waenda kwa miguu kwa sababu hakuna fedha wanasubiri bajeti ya 2016/17. Waenda kwa miguu wanavuka barabara kwa kufanya 'timing' na spidi ya mhusika kuvuka.

Hivi hii nchi inaendeshwaje? Juzi IGP kasema mashine za utambuzi wa alama za vidole ziliwekwa zote na Lugumi katika vituo vya polisi kama mkataba unavyoonyesha na kwamba zisizofanya kazi ni kukosekana kwa internet katika maeneo hayo, uongo mtupu.

Na leo kwenye taarifa ya habari ya Star Tv ya saa mbili usiku huu nimeona mtu mmoja sijui ni wa Tanroads, Sumatra au polisi akitoa maelezo ya taa hizo baada ya watu watatu kuuawa kwa kugongwa na magari katika muda huu mfupi.

Hivi kweli mambo haya yanabuniwa na wataalam au ni mawazo ya wapiga debe?
 
Back
Top Bottom