Wameshafariki watoto wawili , sasa anadai ana mimba tena! Msaada!

Tafadhali usichukue uamuzi wa haraka kiasi hicho maana hata mama mwenye mtoto nadhani anajiuliza sana kuwa ana mkosi gani. Kumbuka mtoto wa kwanza alifariki wakakati akijifungua na yule wa Pili mimba iliharibika.
Fanya uchunguzi kupitia kwa madaktari ili waone kama kuna tatizo linalosababisha lasivyo utahisi kuwa kuna wachawi/mchawi.
 
Kwa jinsi ulivyoandika huu uzi wako; inaonyesha wazi kwamba humpendi huyu binti but unataka tu umtumie kama mzazi wa watoto wako.....over!! Kama ungekua unamuhitaji yeye kama mwenza wako katu usingewaza kumwacha ati kwasababu ya hayo matatizo ambayo hakuna namna anavyohusika kuya-create, zaidi nae anaumizwa nayo. Jifunze kupenda kwa dhati, jifunze uvumilivu na ujenge imani kwa Muumba (Mungu).
 
ni mawzo yako ndiyo yanayokutesa,jaribu kufikiria mambo mazuri yakumfanyia kiumbe mtarajiwa ,halafu uone matokeo yake kama hujafurahi.mingine hii ni mitihani aisee
 
Pia muombe kabla yakubeba mimba yawezekana hizo mimba xinachukuliwa kichaw au na mapepo au anashida yakihospitali, nikushaur mpelekee hosp ujue tatizo nn afu silaha kuu iwe ni maombi katika maisha yenu
 
Mahusiano miaka mitatu, mimba tatu na bado hujamuoa, Mkuu akijifungua Fanya mpango.
Tena asifanye masihara ...afunge ndoa tu kwanza...asijimilikishe hivyo ....mimba siku hizi hazitabiriki...ikitokea kafariki mama...atalipa mahari na faini juu...nishaona tukio la hivi tena mimba moja tu ilikua...
Kijana mwingine msichana wake kila akibeba mimba zaharibika...huyu jamaa hakukata tamaa alizidi kumpenda na akawa anamsindikiza kwa madk kujua nini tatizo...akamuoa haikuchukua miezi mimba..now ana kibby....
 
Pole sana mkuu! Usikate tamaa! Fikiria maumivu anayoyapata mwenzako. Yeye ndo alibeba hiyo mimba kua karibu nae sana na mfariji. Inaweza kua hayuko vizuri kimawazo na kupata mimba nyingine ndo faraja kwake. Ukimwacha tu hivyo haitakua utu. Kama unampenda kweli usimwache mda huu.
 
Kaka fanyani vpmo vya Rh factor na kama ana group blood -0 mara nyingi kuzaa kwao ni shida hayo ni matatzo ya dunia .Tafuta wataalumu wa afya wachunguze afya zenu kwanza.

Mungu awaongoze na akupe upendacho ila uckate Tamaa kjn
Kweli hili nalo tatizo! Kama rhesus factor haziendani ata mkizaa watoto kumi wote wanaeza fariki! Kachekini hii.
 
Kaka kwanza ukimuacha haitakua suluhisho pia unatakiwa kutumia busara katika maamuzi yako haujafunga nae ndoa then unamgegeda mtoto wa watu mpaka anapata mimba Mara tatu bado hujafunga nae ndoa tuh sio fear kaka.


Anyway ningekushauri nenda hospitals onana na madaktari bingwa ambao wataisaidia familia yako ila usijaribu kumkimbia mtoto wa watu
 
Utakuwa wa dar tu ww, full kupenda njia nyepesi nyepesi! Pambana kijana acha kupenda mteremko, mungu anakupa hiyo mitihan anamaana yake! Huwez jua inawezekana amekutengea nn kizuri! Vumilia na atakulipa kwa uvumilivu wako
 
Huyo atazaliwa mzima salama salamina, kukimbia mke sio suluhu ya matatzo, mkubali na amini ndio wako
 
Dah mbona unamuonea hivo unadhani yeye pia hataki mtoto. Wanaume wengine mnashangaza sana, eti umuache looh. Kuna wanaume wameishi na wake zao miaka yote bila hata ya kuwa na mtoto lakini hawakuwaacha, walivumilia, sembuse wewe matumaini yapo? Acha ujinga, wala hilo lako sio tatizo, ukiwaona wenye matatizo wewee mbona utajishangaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom