Ni kweli Michael Richard Wambura anapambana kuhakikisha anapata uongozi Simba.
Wakati akifanya hivyo, kumekuwepo na nguvu za ndani na nje ya Simba SC. kuhakikisha hapati fursa hiyo.
Kutokana na hali hiyo, sasa ni wazi kuwa iwapo atavuka kikwazo cha sasa Simba itapasuka kwani kuna uwekezaji mkubwa unaofanywa kuhakikisha havuki. Ndiyo, anaweza kuwavutia wanachama na hatimaye akapata cheo anachokihitaji, lakini je, klabu ya Simba, kama Yanga, haijiendeshi bali inaendeshwa moja kwa moja, ama kinyume chake na kundi la wachache. Swali ni je, Wambura anataka aachiwe 'shuzi' la Simba?

sijui wanachomuogopea nn hawa viongozi waliokuwepo,,kama huyo aveva kakaa na rage hakuna jipya anataka nafasi nyingine ya nini tena?
Nashangazwa na wanaomjengea Wambura sifa za kuwa kama ndio mwarobaini wa matatizo ya Simba. Wanasahau kwamba hana tofauti na Watanzania Wanasimba wengine, akiwamo huyo ambaye madonda yakekwenye Simba ndio eti anategemewa Wambura ayaponye, Ismail Rage. Nionavyo, Wambura au bilaya Wambura, Simba ndiyo ileile, kama ilivyokuwa alipopata kuwa kiongozi wake mkuu. Kiongozi bora ni yule anayesaidia kuleta umoja wa anaowaongoza. Kama wanaotarajiwa kuongozwa wameshagawanyika hata kabla hajachaguliwa, anapaswa kuongoza akiwa nje ya uongozi. Si kwa majungu na fitina, bali kusaidia kuleta umoja na maelewano kwa kutumia ushawishi, umaarufu wake. Aliwahi kufanya hivyo Hayati Mwalim Nyerere kwa kumpisha Kawawa awe Waziri Mkuu, yeye akaimarisha TANU ikubaloke zaidi na wananchi. Baadaye si akarejea hadi kuwa Rais wetu (kwa tuliokwishazaliwa enzi hizo). Kama kweli Wambura ana wafuasi anaodhani anao, haraka ya nini?
Inayoitwa 'haki' ya mwananchi/mwanachama kuchagua na kuchaguliwa, si haki ya kuzaliwa kama ilivyo ya kuishi. Ni haki iliyowekwa na Katiba ya nchi/jumuia husika kwa madhumuni ya kuleta maelewano na kuepusha migogoro ndani ya nchi/ jumuia hiyo. Lakini kama 'haki' hiyo inashindwa kufikia lengo hilo hata kanla haijatumika, kuna haja ya kuin'gan'gania? Katiba zipo kuwatumikia watu, sio watu kuwa watumwa wa katiba.hupo sahihi mkuu lakini hasipo tetea haki yake leo hata uko mbele mambo yatakuwa hivihiv i komaa Wambura