Tanzania Prisons 0-1 Simba | Ligi Kuu Bara | Uwanja wa Sokoine | 14/09/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbiringe ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kuendelea kuvurumishwa vilivyo leo September 14, 2022 ambapo Wajelajela Tanzania Prisons, wanawakabili vikali Wekundu wa Msimbazi Simba SC, kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Mchezo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana ushindani ambao unapatikana ndani ya Uwanja kwa siku za hivi karibuni wakati timu hizi zinapokutana. Je kwenye mchezo wa leo nani kuibuka na ushindi? Dakika 90 za Mbiringe kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 Alasiri.. Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

=================

Timu zote mbili zipo uwanjani tayari kwa kuanza kwa mchezo huu wa Ligi Kuu.

Mwamuzi wa katikati ya Uwanja ni Ahmed Arajiga kutoka Manyara.

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Sokoine dakika 90 za jasho na damu | Tanzania Prisons 0-0 Simba SC.

05' mpira ni mkali na mashambulizi ni kwa zote mbili, wakianza kusomana kimchezo, shughuli pevu..!

10' Prisons wanashambulia lango la Simba, lakini shamblluli lao linashindwa kuzaa bao.

12' Simba wanajibu shambulizi, kichwa cha Sakho kinashindwa kulenga bao.

15' Prisons wamenusurika hapa kupigwa bao, Phiri na Kyombo wakichachafya. game imechangamka sana hapa

20' Majaribio mawili ya Phiri yashindwa kuleta bao upande wa Simba SC.

22' Prisons wanashindwa kutumia Krosi ya Ismail Michael, ilikuwa hatari langoni kwa Simba

Golikipa wa Prisons yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupambana na Kyombo, ameinuka mpira unaendelea.

28' Abraham anaonyeshwa KADI ya Njano baada ya kumshika Kyombo, ni faulo kuelekea Prisons.

35' Simba wanakosa nafasi tena, mpira wa Kichwa cha Mkude kinapaa nje ya lango baada ya free kick ya Chama.

41' Kona inapigwa kuelekea Simba, lakini mabeki wa Simba wanakataa, wanamiliki prisons wanapiga mbele ooooh mpira unatoka nje.

45+1 Kuelekea kuwa mapumziko.

Unapigwa mpira mrefu lakini golikipa Manula anacha na kutoka nje na kuwa goal kick

Naaam mpira ni mapumziko.

HT: Tanzania Prisons 0-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza huku Simba wakifanya mabadiliko Ameingia Kibu badala ya Kyombo.

Phiri anaangushwa eneo la box refa anakataa anasema acha janja janja hapa.

53' Inapigwa Kona inamkuta Hussein anapiga shutii lakini golikipa wa Prisons anadaka halafu analala chini.

Phiri anapiga shutii lakini golikipa wa Prisons anadaka halafu unamtoka na anadaka tena, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga.

Massenga anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Phiri

Chama anapiga shutii lakini golikipa anadaka huku Mbangula anakosa nafasi vile vile ya kufunga.

Ameingia Onyango na ametoka Henock na ametoka Sakho na ameingia Okrah

62' Mbangula anakosa nafasi nzuri ya kufunga, mpira wake unagonga Mwamba, ilikuwa hatari langoni kwa Simba SC

Ametoka Mgunda na ameingia Mcha upande wa Prisons

Kona inapigwa kuelekea Tanzania Prisons lakini unaokolewa wanamiliki prisons

65' Chama anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya. Mpira ni kali kwa pande zote mbili.

Okrah anapiga Krosi lakini mpira unatoka nje, Simba wanasaka muhimu hapa.

70' Tanzania Prisons wanakomaa hapa Hussein Abel golikipa wao anakaa imara.

Haya inapigwa Counter Attack kule kwake, Mbangula, kwake Mcha anapiga shutii njeee.

79' Game imebalance yoyote anaweza kupata ushindi ikiwa sasa Prisons wanapata Kona mbili ambazo hazikuzaa bao.

Balua anaingia kuchukua nafasi ya Nyamtini upande wa Tanzania Prisons

Counter Attack kule Balua, wanakosa nafasi ya kufunga Prisons

86' Mkude Goooooooooooooaaal gooal
Goooooaaal

Jonas Mkude anaipatia Simba SC bao la kwanza akipokea pasi ya kichwa ya Kibu

Elfadhili ametoka na ameingia Asukile upande wa Tanzania Prisons

Massenga anaonyeshwa KADI nyekundu, baada kuchezea vibaya Phiri, ni Kadi ya pili ya Njano

90+3' kuelekea kumalizika kwa mchezo, haya mpira wanao Simba SC kwake Chama pembeni kulee

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Tanzania Prisons

FT: Tanzania Prisons 0-1 Simba SC

...... Ghazwat...
 
Naona wachawi mmeingia
Namba hazijawahi kudanganya.

Prisons ni nzuri sana akicheza na Simba endapo yupo Mbeya..
Screenshot_20220914-143038.jpg
 
Back
Top Bottom