Wamasai wanted Morogoro mjini

twatwatwa

JF-Expert Member
Sep 19, 2011
2,067
419
Kufuatia kitendo cha wamasai kumuua kwa kumkata mapanga kijana mmoja wa bodaboda huko katika mashamba ya Mgongola Mvomelo.

Sasa sakata hilo limeamia mjini kila masai anaetia mguu mjini cha moto amekipa vijana wa bodaboda wemejioganaizi popote anapooneka mmasai wanamfanyia ambushi kubwa, jana nilishuhudia wamasai wawili wakila kichapo cha mbwa mwizi mpaka kupelekea kuvunjwa miguu na mwingine kukimbilia katika gesti ya Masinga ambako alikuja kuokolewa na SMG za police.

Eneo lote la Morogoro mjini huwezi kuta mmasai hata mmoja toka jana labda aje amevaa suti na kapelo. Imefikia hata wakijificha kwenye magari ya abiria hushushwa na kupewa kichapo.

Hawa wamasai walipiga na kuua wakulima majuzi huko Mvomero hivyo bodaboda wanalipiza kifo cha mwenzao aliyecharangwa mapanga.
 
Inasikitisha sana....

(Nje ya mada:Mkuu,samahani fanya "editing" kidogo taarifa yako isomeke vizuri.)
 
Hii nayo inapatika Tanzania tuu chini ya uongozi wa Prof,Dr,Dr,Dr,Dr Kikwete
 
ttzo la masai anaamini ngo'mbe ni zaidi ya binadamu na hii imechangia wao kupenda ngo'mbe kuliko watoto wao na kuozesha mabinti wadogo ili wapate mifungo
 
Hizi stereo-type mbaya sana! Sasa mimi kuwa mmasai (kama walivyo wazigua, waluguru, etc) linakuwa tatizo? Mzigua mmoja akiiba basi wazigua wote tunakuwa 'wezi'?
 
Nipo Morogoro kwa sasa kwakweli hali ni mbaya sna wamasai wahatakiwi kuonekana kabsa kutokana na huu uhasamapia kuna tetesi kwamba wamasai toka sehemu mbalimbali za mkoa wa Morogoro wanajikusanya kimakundi kwa ajili ya kuja Morogoro mjini kuonyeshana ubabe!
 
Ni wajibu wako kumlinda (protect) mwananchi mwenzio !! kemea na usimamishe tabia ya mtu kuchangiwa ...!! Uwe raia mwenye uzalendo na utaifa !! Jamanii tulinde amani...sheria zipo, Polisi ipo mahakama ipo, Serikali ipo !! twatwatwa SMU
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom