Wamachinga wapewa kipaumbele

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Waziri wa Fedha Dkt. Mwiguli Nchemba alizungumzia suala la wafanyabiashara wadogo (wamachinga), Dkt. Mwigulu aliwataka waendelee kutulia kutokana na suala la ulipaji kodi kwasababu limeshafika mezani kwa Rais Samia Suluhu.

"Kuhusu matumizi ya mashine ya kieletronicki (EFD) kweli taharuki ilitokea, lakini naomba watulie utaratibu mzuri uendelee kufanyika kwa upande wao."

Lakini aliongeza kuwa Serikali imelenga kuwawezesha wamachinga wote kwa kuwapatia maeneo mazuri ya kuendeleza biashara zao kwa dhamira ya kuhakikisha wanakopesheka maana serikali inaendelea kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu hivyo kuna umuhimu wa kuyatambua maeneo wanayofanyia biashara zao.

Vilevile alisema Lengo la kufanya hayo yote ni kumsaidia Rais Samia Suluhu kutekeleza dira yake katika kuongeza fedha kwa sekta za uzalishaji ikiwemo Kilimo, Uvuvi, Mifugo na mikakatiya kukuza sekta binafsi
 
Wameshindwa kuwafukuza mitaani wameamua kujipendekeza kwao
Kwanini wawafukuze bila kuwapa sehemu ya kwenda ndio maana Serikali ya Rais Samia Suluhu inajenga masoko ya wamachinga ili watambulike na waweze kukopesheka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom