Wamachame wazibeni midomo watesi wenu kwa shuhuda zilizo hai!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,405
7,384
Tokea nikiwa mdogo, nilikuwa nikisikia kuwa wanawake wa Kimachame wana tabia ya kuwaua waume zao pindi wapatapo mali.

Wanasema muda ni hakimu wa kweli! Baada ya kuwa mtu mzima, nimefahamu kuwa si Wamachame tu, bali na makabila mengine kuna mengi wanayohusishwa nayo ambayo kiuhalisia hayana ukweli.

Kuna watu wengi wamewao Wamachame, na sasa ni wazee lakini bado wanaoishi pamoja. Hata Mzee Frederick T. Sumaye mke wake ni Mmachame.

Kwa sababu uzushi huo ungali ukiendelea, na kwa namna moja au nyingine kuwasababishia usumbufu mabinti wa Kimachame, ninawashauri Wamachame wawe wanatoa shuhuhda mbalimbali za wazee wao walioishi na wenzi wao hadi uzeeni. Naamini wapo wengi tu, tena, wengine ni matajiri. Nalijua hilo, nilishawahi kukaa kwa muda Machame.

Kuona ni kuamini! Watu wajioneapo kwa macho yao wenyewe wazee matajiri wa Kimachame, itasaidia kufuta uongo kuhusu Wamachame ambao umedumu kwa miaka mingi.

Ifahamike kuwa hakuna kitakachobadilika bila kubadilishwa. Huo uongo uliotamalaki kwa miaka mingi utafikia kikomo pale ukweli utakapokaa mahali pake.

Naomba kuwasilisha.
 
Wanawake wa Machame ni warembo sana ila hawarushi maji wakati wa tendo
 
Back
Top Bottom