Waliozalisha watumishi hewa kikaangoni

Lenatuschacha

Senior Member
Jul 29, 2015
156
36
k.majaliwa.png


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka makatibu tawala wa mikoa nchini kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliosababisha kuwapo kwa watumishi hewa.
Amesema suala hilo la watumishi hewa limeisababishia Serikali hasara kubwa, hivyo ni lazima watu wote waliohusika katika sakata hilo wabainishwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi iliyowasilishwa na mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi katika siku ya kwanza ya ziara yake ya pili kikazi wilayani Ruangwa.

Wakati akiwaapisha wakuu wapya wa mikoa Machi 15, Rais John Magufuli aliwapa siku 15 kuhakikisha wanabaini watumishi hewa wote katika mikoa yao na kuwaondoa katika mfumo wa malipo.

Baada ya kufanyika kwa kazi hiyo, jumla ya watumishi hewa 7,795 walibainika ambao wameisababishia Serikali hasara ya Sh7.5 bilioni.

Awali, Zambi alisema Lindi ina jumla ya wafanyakazi watoro 57 na hewa saba ambao walifariki na wengine kustaafu, lakini walikuwa wakilipwa mishahara na kuisababishia Serikali hasara ya Sh36 milioni kwa mwezi.



Chanzo:MPEKUZI
 
Ni sahihi; Anne Kilango asiwe muhanga wa zoezi hilo peke yake; waliotengeneza tatizo lenyewe lililosababisha mama wa watu huyu kutumbuliwa kwa kudhalilishwa kiasi hicho waadhibiwe vikali zaidi ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha za umma au kufilisiwa.
Mlipokuwa mnakula jasho la wanyonge mlikuwa mnajiskiaje? Acha mdhalilishwe tu.
 
Kwani serikalini si wanalipia through banks?si wafuatilie nani alikua anachukua hiyo mishahara ya wafanyakazi hewa tu?
 
Ukileta orodha ya Watumishi hewa unaulizwa kwa nini una watumishi hewa? unachukuliwa hatua
Usipoleta orodha ya watumishi hewa kama Mama Lemutuz unatumbuliwa!
Ukilalamika Mafungu Madogo Wizarani unategeshewa tape recorder unatumbuliwa
Ukileta Fyokofyoko unafyokolewa
Wabunge wamedhibitiwa sasa wanarudisha 6 billion.

Ukomo wa Urais kwny Katiba Uondolewe tuweze kufaidi "Pombe".
 
Ukileta orodha ya Watumishi hewa unaulizwa kwa nini una watumishi hewa? unachukuliwa hatua
Usipoleta orodha ya watumishi hewa kama Mama Lemutuz unatumbuliwa!
Ukilalamika Mafungu Madogo Wizarani unategeshewa tape recorder unatumbuliwa
Ukileta Fyokofyoko unafyokolewa
Wabunge wamedhibitiwa sasa wanarudisha 6 billion.

Ukomo wa Urais kwny Katiba Uondolewe tuweze kufaidi "Pombe".
Hii ya wakuwarekodi mawaziri wanaolilia nimeipenda sana....!!
 
Yaan kipindi hiki hata michepuko inaisoma namba.sasa waende msoga wakapate ufadhili
 
wafungwe kabisa, watu wanateseka mitaani kwa kukosa ajira, wao nakula mishahara hewa? Kumbe mtu unapeleka vyeti vyako kuomba hajira majizi yanachakachua na kukuingiza kwenye list ya mwajiriwa, bila wewe kujua na kula mshaara huku wewe ukinyimwa kazi?

Magufuli, funga hao watu haraka sana, na ikibainika wale waliokuwa wanakuja kuomba ajira na kunyimwa kumbe wameajiriwa bila wao kujua na huku wakiwa hawajui, basi wapewe hizo hajira za ao majizi.
 
Back
Top Bottom