Waliotandikwa viboko Ikulu hawa hapa

if this is the argument to go by, the current globalization is killing more than you just mention. Just image the North Mara sagga, the Bulyankuru issues, to mention few. the imperialists' regimes never want a person who wants to liberate the mind of the enslaved. Remember, freedom is a matter of death and life and not a given gift on the golden plate.
 

labda anamhusisha mwalimu in the fact that mwalimu ndio aliidhinisha kifo cha Dr kleruu kwa kusaini hati iliyoidhinisha kunyongwa kwa mkulima Said Mwamindi,bila kukumbuka kua mwalimu alikua under pressure ya wakuu wa mikoa wa kipindi hicho waliotaka mwalimu aidhinishe kunyongwa baada ya mahakama kumhukumu hivyo ili iwe fundisho kwa wengine.
 
mbona umenichanganya mkuu hebu weka sawa hapa!
 
mbona umenichanganya mkuu hebu weka sawa hapa!

i mean baada ya mahakama kumtia hatiani mkulima said mwamindi kwa mauaji ya Dr Kleruu,ili mtu anyongwe ni lazima raisi asaini otherwise hutanyongwa,so mwalimu alisaini thats why Mwamindi akanyongwa
 
i mean baada ya mahakama kumtia hatiani mkulima said mwamindi kwa mauaji ya Dr Kleruu,ili mtu anyongwe ni lazima raisi asaini otherwise hutanyongwa,so mwalimu alisaini thats why Mwamindi akanyongwa

sasa hapo nyerere alimuuaje dr kleruu mkuu?
 
sasa hapo nyerere alimuuaje dr kleruu mkuu?

mkuu sijasema mwalimu alimuua kleruu,ktk maelezo yangu nilisema uyo aliyemhusisha mwalimu na kifo cha kleruu(kuna member mmoja hivi ktk post flani uko juu) labda alimaanisha mwalimu kusaini ndio kamuua yeye.otherwise labda tumeshindwa kuelewana ktk interpretation mkuu.
 
JokaKuu umechemsha,

Mwalimu aliamuru wanafunzi watandikwe bakora. Cha ajabu kipi hapo?

Nani alikwambia mwanafunzi wa chuo kikuu hachapwi bakora akichemsha? Basi hata jera asiswekwe akipatikana na hatia - maana yeye ni mwanafunzi wa choo kikuu.
Adili,

..wanafunzi wa Chuo Kikuu wamepita umri wa kukanywa kwa viboko.

..kwa umri wao wangebaki vijijini wanaweza kuwa na mke/wake na miji yao.

..tena kuna wengine wanaotokea makazini huwa ni watu wazima wenye familia.

..kwa uelewa wangu Mwalimu alijutia kitendo kile cha kuwatandika viboko "wakosaji."

..utaratibu wa kuchapa bakora watu wazima waliovunja "sheria" naamini ulianzishwa na wakoloni.

NB:

..kama wanafunzi wa chuo kikuu amefanya uhalifu basi anastahili kwenda jela kama wengine tulioko mitaani.
 
Last edited by a moderator:
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!

Dogo utakuwa mgonjwa wewe!

JKT imekufa wakati wa Mwinyi. Maana ameanza kutawala 1985 mwishoni hadi 1995 mwishoni. Na watu wa mwisho kwenda JKT ni wale walioenda 1994 mwanzoni. Sisi tuliishia kujaza fomu na kupangiwa makambi, tukitakiwa kuripoti mwezi Januari 1995 (hii naikumbuka sana) lakini kwa mshangao wa wengi JKT ikawa imevunjwa. Tumb..ff zao walioshiriki kuivunja!!

Sema wewe kama ulienda hii ya vijana wa kujitolea lakini siyo ile tuliyokuwa tunatoka moja kwa moja High schools na vyuo vya kati kwenda JKT.

Rekebisha kumbukumbu zako dogo!
 

nakubaliana nawewe hapa Bluray umechambua vizuri sana. ila sioni tatizo la vijiji vya ujamaa. kwa sababu ilkuwa ni vigumu kwa wakati ule kuwafikia watu kirahisi kwa sababu walikuwa scaterd.tulitakiwa kwanza kuinvest katika miundombinu then taratibu tuwakusanye wtu katika vijiji ili rahisi kuwapatia huduma za kijamii
 

Tata,nakuchukulia kwamba angalau umekwenda shule,kila jambo lina faida na hasara. Binafsi bado naamini kwamba ni kupitia ktk jeshi kama JKT na wanafunzi wa shule za sekondari kusoma mbali ya maeneo walipozaliwa,nchi iliweza kuwa moja. Lilikua zoezi ghali lakini lilisaidia nchi kufika hapa tulipo. Tujiulize leo licha ya maendeleo makubwa ya tekinolojia ya mawasiliano,tunapendana? Tuna amani? Ninachokishuhudia kila siku ni kwamba tunazidi baguana. Chuki na matabaka yametawala. Ikizuka vita leo,gharama ya kurejesha amani itakua maradufu kuliko tungeendelea na mambo kama haya yaliyo waunganisha vijana kama Watanzania.
 
Siyo kweli. JKT ilikufa mwaka 1994

Mkuu,
Asante kwa masahihisho..Mi nilipiga 'Operesheni Vyama Vingi'..

Duh, nimekumbuka ile miraba ambayo ulikuwa ukibisha hodi kwa mtu, basi yenyewe imeshaingia..
Nimekumbuka na zile 'greenvesti za kijani' na yale makapluta...

Zaidi ni nimekumbuka 'disko aisee'... hivi 'Isabela alipatikana mpaka leo'

Natamani kuanzia 2015 kutakapokuwa na utawala mpya, sheria mpya ije ili akina Ritz, Rejao, Chama, thatha, n.k.
 
I once heard that there is a book titled THE DARK SIDE OF JULIUS NYERERE. Where can I obtain a copy please?
 
Julius Kambarage Nyerere , Mwl 1961-1985
Alhaj Ali Hassan Mwinyi ,Dr 1985-1995
Benjamin William Mkapa , Bro 1995-2005
Jakaya Mrisho Kikwete ,Dr 2005 to date
 
naona alifanya vizuri sana maana maadili kwa sasa ni F kabisa yaani naomba utawala wa Nyerere urudi kama mtu anagomea kuhesabiwa (sensa) hawa walitakiwa kuchapwa viboko tena sikuile ile waliyokuwa wanatangaza hawatahesabiwa ndio maana mpaka leo hii serikali imeingia gharama ya kuongeza muda kwa ajili ya kundi la wahuni wachache
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…