Sioni tofauti yoyote kati ya Mwanaidi Maajar na hao wengine. Kama kigezo ni kuwa 'product' ya CCM, basi wote uliowataja ni majanga... Sipingi kuwa na mwanamke Rais, ila sijaridhishwa na yeyote kati ya hao. Huenda siku zijazo tutapata wanawake kwenye nafasi hiyo, lakini sidhani kama tutapata mama mwenye vigezo hivyo hivi karibuni. Wote wamejikita kwenye siasa za vyama na mipasho badala ya kuweka utaifa mbele. Wameacha hata kumtetea mwanamke wa kitanzania na kuweka maslahi yao binafsi mbele. Katika hao wote hakuna hata anayestahili kupendekezwa. Waendelee kupigana vijembe na Sophia Simba kwenye Jumuia yao UWT ambayo imeshindwa hata kumkomboa mwanamke wa kijijini. Wamebaki kushindanisha sura, mavazi na mipasho!