Ulikuwa mshindi halali kura za maoni lakini watawala wa juu wakakukata jina lako na kumuweka mtu wanayemtaka.
Kisha mliokatwa mkaambiwa muwapigie kampeni hawa mahasimu wenu kwa ahadi kwamba mmeshafanyiwa vetting mtateuliwa kwenye nafasi zingine.
Kataeni ujinga huo, yani aliyekukata usigombee baadae aje akuteue?
Inakuingieni akilini kweli, kwanini asingemteua huyo aliyempenda na kumpa nafasi yako uliyopewa na wananchi?
Wanasema mlitoa rushwa, sasa kama hilo ni doa tayari huo uteuzi mtaupataje?
Fanyeni maamuzi sasa, nendeni vyama vingine mkagombee kama mnaamini mlishinda na mtashinda nafasi za kuchaguliwa.
Kumbukeni hizi za kuteuliwa ni kama mwanamke anayechumbiwa, hana uhakika wa kuolewa mpaka siku ya kufunga ndoa.
Na ndio maana huona wanawake hulia siku ya ndoa, hawaamini wamefikia hatua hiyo.
Jitoeni CCM nendeni CHADEMA, ACT au chama chochote mkathibitishe hamjatoa rushwa na mlionewa ili wananchi wachague, huko CCM hata mkibaki mmeshatuhumiwa kwa rushwa, sasa mtateuliwa vipi?
Muda ndio huu msichelewe kwa ahadi hewa mtajuta.