Uchaguzi 2020 Walioshinda kura za maoni na kukatwa, msikubali ujinga huu

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
8,689
11,277
Ulikuwa mshindi halali kura za maoni lakini watawala wa juu wakakukata jina lako na kumuweka mtu wanayemtaka.

Kisha mliokatwa mkaambiwa muwapigie kampeni hawa mahasimu wenu kwa ahadi kwamba mmeshafanyiwa vetting mtateuliwa kwenye nafasi zingine.

Kataeni ujinga huo, yani aliyekukata usigombee baadae aje akuteue?

Inakuingieni akilini kweli, kwanini asingemteua huyo aliyempenda na kumpa nafasi yako uliyopewa na wananchi?

Wanasema mlitoa rushwa, sasa kama hilo ni doa tayari huo uteuzi mtaupataje?

Fanyeni maamuzi sasa, nendeni vyama vingine mkagombee kama mnaamini mlishinda na mtashinda nafasi za kuchaguliwa.

Kumbukeni hizi za kuteuliwa ni kama mwanamke anayechumbiwa, hana uhakika wa kuolewa mpaka siku ya kufunga ndoa.

Na ndio maana huona wanawake hulia siku ya ndoa, hawaamini wamefikia hatua hiyo.

Jitoeni CCM nendeni CHADEMA, ACT au chama chochote mkathibitishe hamjatoa rushwa na mlionewa ili wananchi wachague, huko CCM hata mkibaki mmeshatuhumiwa kwa rushwa, sasa mtateuliwa vipi?

Muda ndio huu msichelewe kwa ahadi hewa mtajuta.
 
Usiwavunje moyo chama cha mapinduzi na serikali yake kuna nafasi nyingi ya uongozi
 
Usiwavunje moyo chama cha mapinduzi na serikali yake kuna nafasi nyingi ya uongozi
Hahaha yani ufae wapi kama ubunge hufai?!

Na aliyekukataa unataka akuteue wapi?!

Usiwapumbaze, waliopaswa kuteuliwa ni hao waliopendwa na kupewa nafasi za kugomnea ambazo hawakustahili.
 
Mshauri ivyo na yule mama wa cdm jimbo la segerea alishinda kula za awali ila kawekwa mwngine alishindwa
 
Mkuu, in 62 months, these people will be gone.. These vacancies will again be up for grab... Sasa kwa nini ujipe presha? Hiki ni kipindi cha kujipanga tena for 2025kwa wale wote waliokosa.
Bora ujipange nje ya ccm, kule wakiisha kupa label fulani hutoboi.

Ukiitwa ni mpambe wa membe, usubirie mpaka 2026, au wakikusingizia ulitoa rushwa ni hivyo hivyo usubirie 2026.

CCM wote wamejipitisha kwa hila na mapenzi yao, mlioachwa hamtakiwi ccm, mnasubiria nini?!

Vyeo tayari wapo waliotii maagizo ya Maguful kwamba wasiende kugombea na hawakwenda, walioenda wamefukuzwa isipokuwa wachache kama Mpango na Ndalichako, au Hussein Mwinyi.

Sasa mwenzangu na mimi unasubiria nini ccm?!
 
WAJUMBE tupo pamoja sana. Ninyi ndiyo mnaowajua fika WATIA NIA na mnaishi nao mtaani. Siyo NEC. Kutoheshimu uamuzi wenu ni kosa kubwa sana na dharau iliyokithiri. Sasa mna kura moja ya turufu. Ni kutowapigia kura ya NDIYO Oktoba 28.
 
Back
Top Bottom