1979Magufuli
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 439
- 1,756
Uwanja wa Taifa ni juzi tu umetoka kukarabatiwa na sasa uko kwenye kiwango, hakuna ubishi kuwa gharama kubwa imetumika kukarabati uwanja huo na kuuletea heshima kubwa nchi.
Sasa Leo inaonekana mitandaoni kuwa Yanga wametumia geti lisilo rasmi kuingia uwanjani ili kucheza na Simba, imani zao za kijinga kuwa wamerogwa na wakipita sehemu ya kawaida watafungwa, hii ndio timu inayojinasibu kuwa ni professional, ni timu ambayo mwenyekiti wake ameonekana akiwaswalisha wachezaji wake ili kukidhi masharti ya waganga, yaani kiongozi mkubwa wa utopolo anatumwa na waganga kuswalisha wachezaji ili tu kuifunga Simba!
Swali langu, nani amewafungulia Utopolo geti lisilo rasmi wakati inajulikana kabisa kuwa wote tunatakiwa kupita geti moja? Hamuoni huo ni uharibifu wa uwanja? Walipata wapi ufunguo? Nani alikuwa na mawasiliano na uongozi wa uwanja? Kwanini vitendo hivi vinajirudia mara kwa mara licha ya adhabu kali kutolewa?