Waliomuua Dk. Mvungi kuanza ‘kukaangwa’

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,248
2,000
UPELELEZI wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya Dk. Sengondo Mvungi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umekamilika.

Mbele ya Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu, Pamera Shinyambala ambaye ni wakili wa serikali, amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo ameiomba mahakama ipange tarehe kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya mashahidi.

Miongoni mwa washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Chibago Magozi (32), John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).

Katika orodha hiyo yumo pia Longishu Losingo aliyekuwa mlinzi wa Dk Mvungi, dereva na mkazi wa Kitunda, Masunga Makenza (40) ambapo kesi hiyo itaendelea tarehe tena tarehe 29 Desemba 2016.

Inadaiwa kuwa, kwa pamoja watu hao walimshambulia kwa mapanga na hatimaye kumsababishia kifo Dk. Mvungi mnamo tarehe 3 Novemba, mwaka 2013. Wanadaiwa kufanya kosa hilo la mauaji kinyume cha kifungu cha 196 cha Sheria na Kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
 

STDVII

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,585
2,000
Umeambiwa ktk orodha hiyo "yumo pia Longisho Losingo aliyekua mlinzi wa Dk Mvungi na Masunga Makenza aliyekua Dereva wake" zaidi ya hapo tunataka nini?
 

Mthuya

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
1,415
1,225
Hihi nnchi kuna mambo yanafanyika hata shetani awezi kushuudia ila kunasiku yatafika mwisho
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,392
2,000
mambo wehu huaminiwa na wehu

hii ni hadithi ya wehu wa ccm na itaminiwa na wehu wa ccm.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,060
2,000
Wanachekesha hawa ,hao mafundi mwashi sijui wa Vingunguti ndio waliomuua Mvungi ? Hivi fundi mwashi anaanzaje kwenda kumuua Mvungi ? It doesn't add up kabisa

Ndiyo yale yale ya Mkenya gani sijui kumteka Ulimboka

Masterminds ni kina nani ?
Hiyo inatokana na mtuhumiwa alivyoandika katika karatasi yake ya maelezo.
Ndio maana kuna kipenfele cha "ONYO" kwa hayo maelezo yanawezeka kutumika dhidi yako
Kwani ili uuwe unatakiwa uwe baunsa au askari mkuu?
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,203
2,000
R.I.P Mvungi naamini Mungu amekuweka pema kwa kuwa hukuwa mnafiki, pole yao kina polepole kwa uwa na ndimi mbili ole wao siku ya hukumu maana imeandikwa bora uwe moto au baridi, ukiwa vuguvugu nitakutapika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom