Waliompiga Daktari mkoani Mtwara wakamatwa wakijiandaa kutoroka kwenda nje ya nchi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara,Henry Mwaibambe amesema hadi sasa watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya Mkoa wamekamatwa usiku wa kuamkia jana wakitoroka nchini huku wengine 3 wakiendelea kusakwa.

Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi

Jana, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliweza kufika Hospitalini hapo na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa watumishi hao wa Afya.
 
Wapigwe tu! Hamna namna. Mwezi uliopita walichukua pesa ya mtu pale temeke kwa ajili ya x-ray kumbe mashine mbovu jamaa alipogundua akapiga kichapo madokta 2 kisha akarudishiwa hela yake na kusepa.
 
Mmmmh!Kumpiga mtanzania yoyote hata kwa sababu yoyote kubwa kiasi gani sio jambo la kusherehekea hivi tukianza kuseto disputes katika jamii kwa njia ya kupigana itakuwa jamii ya aina gani? and where is the rule of law!????????.
 
Na hao madokta wawe waungwana na wenye kauli nzuri ....wakiendeleza style hiyo ya kutowasikiliza wagonjwa kwa kuendekeza rushwa na tamaaa wataendelea kupata kipondooo tu
 
Wapigwe tu kwa kweli. Kuna cku nilikuwa nina mgonjwa wangu pale muhimbili..kweli nilitamani kupigana na wale manesi lakini nikaogopwa nisije nikadundwa mie maana kupigana sijui. Naomba wenye nguvu wawapige tu kama watakosea lakini.
 
Wapigwe tu kwa kweli. Kuna cku nilikuwa nina mgonjwa wangu pale muhimbili..kweli nilitamani kupigana na wale manesi lakini nikaogopwa nisije nikadundwa mie maana kupigana sijui. Naomba wenye nguvu wawapige tu kama watakosea lakini.
Hivi mnajua kama wenye hii taaluma ni wachache sana, tutakufa kama tutashindana nao, ila ninachoona ni kwamba wananchi sasa hivi wana nguvu na kiburi kwa vile Rais anawapenda sana wananchi na kuwaonea huruma, unajua hata mkiewa kwenye family kama baba anawapenda sana wale wadogo wa mwisho ujue hawa wadogo watakuwa kiburi kwa kaka zao wakubwa au dada zao...SI KWAMBA BABA AMEWATUMA WAFANYE HIVYO ILA WANAJIONA WAKO SALAMA ZAIDI. Rais hajawatuma ila fikra za wananchi kwa sasa wengi wanaona ni wakati wao sasa kutamba mana alieopo anawapenda, kuwajali na kuwaonea huruma, Nadhani wanachi tupigane na majambazi na mafisadi hawa madr. si vyema kuwavunjia heshima na kuwadhalilisha japo na wao wana kasoro zao na uzembe wao katika kazi.
 
Wawapige na polisi pia
Kama kuna watu wa kuchapa nchi hii ni hawa wengi wa mapolisi kwa kukithiri kwa rushwa, kubambikiza kesi nk.
Japo na ma dr. Baadhi wanakera lakini kwa hili la
Mtwara halikubaliki, je! Walitika huduma gani ikiwa hosp haina uwezo wa huduma hiyo?
Wakulaumiwa ni serikali kutoziwezesha hosp kutoa huduma stahiki. Madaktari wa hosp za umma wana mateso makubwa kwani hawana vitendea kazi kabsaa
 
Back
Top Bottom