Waliokuwa waasi wa GADDAFI waingia Mali.

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
17 Oktoba 2011 11:45

Wapiganaji wa kabila la Tuareg waliorudi Mali
kutoka Libya wanaaminika kusaidia katika
kuanzisha kundi jipya la waasi. Kundi hilo la National Movement for the Liberation
la Azawad NMLA limesema ni matokeo ya
muungano baina ya makundi mawili ya waasi,
yaliyoongezwa nguvu na Watuareg waliopigana
kwa ajili ya Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya. Watuareg wa Mali wamelalamika kwa muda
mrefu kwa kutengwa na serikali ya kusini. NMLA wanataka uhuru wa eneo la jangwa
kaskazini mwa Mali. Watuareg ni jamii ya kuhamahama ambao
aghlabu huishi katika jangwa la Sahara na karibu
na miji kwenye nchi kaskazini na magharibi
mwa Afrika. Tangu mwanzo wa mgogoro wa Libya Mali
imekuwa ikisema kuanguka kwa Kanali Gaddafi
kutaathiri utulivu eneo hilo. Mwandishi wa BBC Martin Vog kwenye mji
mkuu, Bamako, amesema jambo linalotokea sasa
ni sababu ya Mali kuunga mkono nafasi ya Libya
kwenye Umoja wa Afrika, ambayo ilipendelea
kutatua tatizo lililopo kwa mazungumzo badala
ya kampeni ya kurusha mabomu inayofanywa na Nato. Mwandishi wetu alisema Watuareg wenye ndoto
za kuwa na uasi mpya wameamua kutumia
wakati huu, kwa kurejesha kaka zao wenye
silaha madhubuti na wenye mafunzo thabiti,
kuonyesha msimamo wao halisi. Alisema matakwa yao ni yenye uzito zaidi kuliko
makundi ya waasi wa awali.
Source:BBC
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom