Waliofaulu usaili ajira serikalini kufutwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Watu wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya ajira serikalini kupitia Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya ajira kusimamishwa, watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi ajira hizo zitakapotangazwa tena.

Waziri wa Utumishi na Utawala Bora
Hilo limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia majibu kwa wadau mbalimbali kwa mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa kila mwezi kupitia tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo litawahusu wale ambao walifaulu usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya kazi au kupewa barua na waajiri wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki wa watumishi hewa.

Taarifa hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo, kwamba majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.

"Kwa mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita" Imesema taarifa hiyo.

Swali lingine kutoka kwa mdau na jibu lake liko kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa ajira zilisitishwa mwezi Juni, na sasa ni mwezi Desemba, utaratibu huo unamaanisha kuwa wasailiwa wote waliofaulu lakini hawakupangiwa kazi, watalazimika kusubiri upya matangazo ili waombe upya na kufanya usaili upya.

Aidha Sekretariet hiyo imebainisha kuwa zoezi ya uhakiki wa watumishi hewa bado linaendelea, na kwamba wakipewa ruhusa ya kutangaza ajira wakati wowote watatangaza.
 
841aa8ce950978852c985b64fa24d8db.jpg


Source .EATV
 
Hao washazoeleka na tushawachoka na kuwapotezea, labda waje na jipya sasa.
 
Mbona taarifa imekanushwa.. Au itakuwa ikiwa kweli wanatokea wengine wanajifanya kukanusha..
 
Kale kausemi ka "bora ningezaliwa mbwa ulaya" kalipotea miaka miwili mitatu apa,nadhani katarudi soon...just kidding
 
Hahahhhahah sasa ngoja nikatafute cherehani nianze kushona maana naona imekuwa too much
Mchina kashashusha mzigo wa bei chee kariakoo. Bei ya mashono unapata nguo nzuri inayofit vizuri.

Kabla ya kununua cherehani anza fitina ili nguo za China zisiingizwe nchini.
 
Back
Top Bottom