chochote atakachokiandika Kiranga humu hutakiwi kuonesha dalili ya kukipinga.
Kiranga mwenyewe anajipinga katika Hegelian dialectics.
Ukianza kwa kutaka kutompinga Kiranga, ushampinga, kwa sababu Kiranga ni muumini wa kupingana, hata kama ni kupingana bila kupigana.
Chuoni kwenye somo la falsafa nilikuwa nampinga sana mwalimu wangu, I mean nilikuwa nampinga mpaka nooma, mpaka kuna demu mmoja akaniita na kuniuliza unavyompinga unampinga kwa ligi tu au unamaanisha kweli?
Nikasema namaanisha kweli ( ilikuwa mostly mambo ya atheism na kupinga dominance ya western culture, I mean unaingia darasani siku ya kwanza unapewa scope ya darasa unaanza kui criticize scope ya darasa na syllabus). Basi kwa fikra za kibongobongo wakati huo ndo naanza chuo mtoni, nikafikiri professor atanifelisha.
Siku mbili kabla ya mtihani wa semester professor kanitumia email ananiambia nisije kufanya mtihani, nikamuuliza imekuwaje (nikaanza kufikiri niliyotabiri yanatokea, anataka kunifuta kwenye darasa lake nini?).
Mnyamwezi akaniambia wewe ma argument yako yamo kwenye syllabus za graduate level (wakati huo nipo undergrad) . Class participation na coursework zishakupa A+ hivyo huhitaji kuja kufanya mtihani wa mwisho.
Nikaona duh, mnyamwezi mwisho. Yaani anathamini dissenting views kiasi kwamba ingawa hatukubaliani kimaoni ( yeye alikuwa a conservative judge, a Bushite from upstate NY, mimi nilikuwa a left leaning atheist from a country he couldn't pronounce), lakini ali value arguments zangu na kuzikubali enough kunipa A+, bila ya kufanya mtihani wa mwisho.
Kwa hiyo, to the contrary, mimi nathamini mjadala. Nimekaa na watu wanathamini mjadala na kupingana. I subscribe to the Wall St Journal even as I am leaning left, if only just to keep tabs on the empire.
As long as mjadala wa kupingana haujajaa ujinga sina tatizo tukipingana.