'Walioandika matusi mitihani kidato cha nne wapimwe akili' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Walioandika matusi mitihani kidato cha nne wapimwe akili'

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Feb 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Ukonga (CCM), Eugen Mwaiposa, ameitaka Serikali kuwapima akili watahiniwa wa kidato cha nne waliaondika matusi na nyimbo za bongo fleva katika karatasi za majibu ya mitihani yao ya taifa ya kuhitimu elimu ya sekondari.
  Mwaiposa alitoa wito huo jana bungeni wakati katika swali lake la nyongeza kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
  Alisema kitendo cha wanafunzi kuandika matusi ni kisicho cha kawaida hivyo haiwezekani kuwaacha bila ya kujua matatizo yao.
  Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa alithibitisha kuziona baadhi ya karatasi za wanafunzi ambazo ziliandikwa matusi tofauti na alivyotarajia.
  Hata hivyo, Dk. alisema Serikali imeamua kutowafutia matokea yote wanafunzi hao na badala yake imefuta kwa masomo ambayo waliandika matusi na nyimbo hizo.
  “Naomba niwaambie kuwa tumejipanga kuikomesha tabia hii kuanzia kipindi cha mwaka 2012,” alisema
  Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Susan Lyimo, alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kwa walimu waliosaidia kufanya udanganyifu kwenye mitihani ya wanafunzi wa darasa la saba katika mitihani ya mwaka 2011.
  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo alisema serikali imekuwa ikichukua hatua mara tu yanapojitokeza matatizo kama hayo.
  Mulugo alisema kutokana na udanganyifu wa mitahi hiyo, wizara imewashusha vyeo baadhi ya walimu ikiwa ni pamoja na kuwazuia kusimamia mitihani.
  Alitolewa mfano kuwa katika adhabu hiyo, walimu nane wa Mufindi walikumbwa na adhabu, Mbeya watano, Ruvuma nane Jiji la Dar es Salaam 18 .
  Alisema serikali iliunda tume kwa ajili ya kuchunguza jambo hilo kwa kina na majibu ya tume hiyo yanatarajia kutolewa Aprili mwaka huu na kutoa adhabu kali kwa kwa wahusika.
  Katika hatua nyingine; Mulugo amewataka wabunge na wanaharakati kuacha tabia ya kuwaonea huruma wanafunzi wanaopewa adhabu kutokana na udanganyifu.
  “Naomba mtuache tufanyekazi nyinyi ndiyo mnaowaonea huruma hawa watoto…napenda kuwaambia kuwa adhabu za kufutia matokea na kuwasimamisha kutofanya mitihani zitaendelea kwa wanaobainika,” alisema  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwa gharama za wazazi au serikali?
   
 3. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,754
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Kama mtihani mgumu unafikili wataandika nini................
   
 4. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Akili zao ziliishia hapo. Acha warud mtaani ulimwengu uwafunze
   
 5. n

  nhassall Senior Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wape njia za kujifunza huko mtaani utawasaidia zaidi
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asome majibu ya JK DAvos halafundo ajifikirie upya nani wa kupimwa akili..hebu anipishe hapa ...mijitu mingine bana
   
 7. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,657
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Usitetee ****** wa walichokifanya watahiniwa hao. Mtihani mgumu ni upi? Inakuwaje wenzao wa shule moja, darasa moja, walimu haohao wafaulu wao uwe mgum? Tusipende kulaumu tu, akili zote zimehifadhiwa Facebook na studio za kurekodi muziki. Ukweli ni kuwa pamoja na mazingira mabaya ya Kayumba zetu ni kweli pia kuwa wanafunzi wa shule hizi hawana utamaduni wa kujisomea. Nenda shule za boarding uone wanaume wanavyo jisomea chini ya miti after school hours. Je hawa wa days wanafanya hvyo majumbani kwao?
   
 8. rifwima

  rifwima JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  sasa alitaka waandike nini kama walikuwa hawakufundishwa wala kusoma? Watibu chanzo cha tatizo siyo matokeo ya tatizo.
   
 9. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Hivi unadhani huko kakora, mpitimbi, Ileje na Nakapanya kuna hiyo FB unayoihubiri?
   
Loading...