Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,607
Mkuu wa Wilaya ya ilala, Sofia Mjema amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala kuwachukulia hatua askari wake wanaochukua rushwa kutoka kwa waendesha bodaboda.
Pia, amesema kuanzia jana vikundi vya ulinzi shirikishi visiwakamate waendesha bodaboda hao, hivyo jukumu hilo litafanywa na wataalamu ambao ni polisi. Hatua hiyo imekuja baada ya waendesha bodaboda wa wilaya hiyo kulalamika kuwa, kuna baadhi ya polisi wamekuwa wakiwaomba rushwa na kuwachapa viboko wanapokuwa wanaendesha pikipiki.
Mjema alisema polisi wanatakiwa wafanye kazi kwa weledi, hivyo yeyote atakayebainika achukuliwe hatua kali za kisheria. “Nasikia wengine wanawachapa viboko, hivyo namuagiza kamanda wa polisi kuwachukulia hatua haraka wahusika wote,” aliagiza Mjema.
Pia, alisema ulinzi shirikishi hawatakiwi kuwakamata waendesha bodaboda hao, hivyo kutokana na kushindwa kazi hivyo itafanywa na polisi.
Mjema alisema vikundi vya ulinzi shirikishi vinatakiwa kufanya kazi zingine, ikiwamo kuwafichua wahalifu.
Pia, walilalamikia Madalali wa Kampuni ya Tambaza Action Mark, wanapotaka kuwakamata kuwa wanawkimbiza au kumkumbatia jambo ambalo linasababisha ajali.
“Nilishaongea na kiongozi wa Kampuni ya Tambaza atoe elimu kwa watumishi wake, wanapokaa sehemu husika wanatakiwa kuambatana na polisi ndiye mwenye mamlaka ya kuwakamata bodaboda siyo wao,” alisema Mjema.
Mkuu wa Kikosi cha Polisi Mkoa wa Ilala, Mashishanga Mwambambiti aliwataka waendesha bodaboda hao kumpelekea majina ya polisi wanaochukua rushwa huku wakiwa na vielelezo ikiwamo kuwapiga picha.
Aalisema bodaboda hao watakapoleleka vielelezo atavifanyia kazi kwa kuwa anayo mamlaka ya kuwachukulia hatua polisi hao.
Mwakilishi wa Umoja wa Bodaboda wa Wilaya hiyo, Peter Kassalu alimuomba Mjema kuwasajili ili walipe kodi ya mapato. Ilala ina bodaboda 50,000.
mwananchi