Walimu Wasiogoma Si wasaliti.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu Wasiogoma Si wasaliti..

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by zubedayo_mchuzi, Jul 31, 2012.

 1. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  jana nimepita shule nyingi za dodoma nikakuta kuna mgomo wa walimu,baadhi yao wakasema walimu wasiogoma ni wasaliti,Nikawakatalia kuwa si wasaliti,mwalimu amefundisha miaka 30 nyuma,amebkiza miaka 2 astaafu leo mnamwambia agome Atagoma huyu? hapo anatetea Maslah yake kundi hili lisiguswe kbs,na hawataki kupoteza Haki zao...gafla nikatoweka na walimu wa 3 wa kiume wakitaka kuwapga walimu waliogoma kugoma ambao ni watu wazima sana,Niliwambia jambo moja tu,Anaejiona Yeye mwamba Awaguse walimu hao...Nilishajawa na U van dame na wangejuta.
  Hakuna kulazimishana kugoma,mtu agome kwa kuifata akili yake ilivyo mtuma na si kwa ku lazimishwa.Si wote wadai haki kwa Mabavu ,Wengine wanalalamia Tumboni na kusubiri miujiza.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Jana Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kuanza rasmi kwa mgomo wa walimu baada ya wengi wao kupiga kura ya kuunga mkono kufanyika kwa mgomo huo.

  Nina maswali kadhaa ya kujiuliza, na sijui wengine mnalionaje hili:

  Kupiga kura ya kuunga mkono au kutokuwa na mgomo ilikuwa ni haki ya kila mwalimu aliye mwanachama wa CWT. Swali langu ni je Wale walimu ambao hawakuungana na wenzao katika mgomo huo ni halali kuchapwa vipoko na wenzao wanaogoma? kama si halali , hawa waliotenda kosa la kuwachapa wenzao wanaweza kuchukuliwa hatua? Je Chama cha walimu kinatoa tamko gani kuhusu hawa wanachama wao waliowapa uhuru wa kuchagua ama kugoma au kutogoma na sasa wanadhalilishwa kwa kuchapwa viboko?

  Vyombo vya habari vimeripoti kuwa katika mkoa wa Pwani na pengne na mikoa mingine , baadhi ya Shule, wanafunzi wamehamasishwa na Walimu kuandamana. Je mgomo huu ni pamoja na Wanafunzi ? au walimu pekee? na kama wanafunzi nao wanahamasishwa kuandamana je nao walipiga kura kuunga mkono mgomo kufanyika?

  Mawazo yangu: Nibora Walimu wakaendelea na mgomo bila kuwahusisha wanafunzi kwani kitendo hicho hakiwatendei haki watoto wadogo hawa ambao hawaelewi hasa nini kinachoendelea kati ya Walimu wao na Serikali yao. Aidha , kwa maoni yangu, ni bora uhuru wa pande zote waliogpma na ambao hawakugoma ukaheshimiwa kwani kusingekuwa na Demokrasia hiyo basi kusingekuwa na haja ya kupiga kura ya ama kuunga au kutounga kuwepo kwa mgomo huo.
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Collective bagaining principal. Walitakiwa wakae kimya nyumbani, sio kuvuruga harakati za walio wengi. Kuwachapa, ni kesi ya jinai, wanaweza kwenda kulalamikia waliowachapa
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mimi nawashangaa sana hawa CWT, hivi kulikuwa na haja gani ya kupiga kura? kura maana yake ni ndiyo au hapana , sasa kama walimu wanapiga kura ya hapana halafu wanachapwa viboko na waligoma, nadhani ni knyume kabisa na maadili ya kazi, na kuna haja ya Serikali kuwachukulia hatua hawa walimu wanaopiga wenzao na ikibidi wafikishwe mahakamani kwa kutenda kosa la jinai.
   
 5. D

  DR. RICHARD Senior Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Si sahihi wao kuwachapa wenzao, lakini pia si sahihi kwa walioamua kutokugoma kujitokeza hadharani kuwapinga wenzao kwani wote wametumia demokrasia yao ya kukubali au kukataa, lakini pia cha kujiuliza hapa ni je wakitimiziwa madai yao je hao ambao hawakuungana na wenzao ni kweli watazikataa nyongeza hizo?
  Hili la wanafunzi, hii ni kwa sababu serikari yenyewe hupenda kuingiza mambo ya siasa katika mambo ya msingi, kwa mfano, tunasikia kunaform zinapitishwa mashuleni kwa lengo la kuwatisha walimu kwa kujaza taarifa zao ambazo hawajui ni za nii?
  pili serikali inatishia kutokuwalipa mishahara wale wanaoshiriki mgomo, sasa swala si liko mahakamani kama wanavyo dai, je huoni wanaingiza na wao siasa, wangeacha mahakama ndo iamue nini cha kuwaanya walimu hao kama kweli wamekwenda kinyume na sheria.
  Vile vile utakumbuka wakati wa mgomo wa madaktari umoja wa vijana wa ccm waliojiita kama wanaccm kutoka vyuo vuikuu waliandamana hadi Lumumba kuwataka madaktari warudi kazini, je ni nanai anauhakika walitumia utashi wao kama si kutumiwa.
  kwa mlolongo huo basi, ndo maana waalimu nao wanfanya hivyo ili kuweza kupaaza sauti zao kwani wanajua serikali inambinu chafu.
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Kugoma na kutokugoma vyote ni haki za msingi ambazo hazipaswi kudhibitiwa kwa mabavu.
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  ila mwaka huu sisiemu kazi ipo
   
 8. M

  MTK JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280

  Mind you the world is ruled by a MOB; comprising of a few crafty people who can move the world to achieve their VISION! thus said;
  "Any successful revolution is achieved either by PERSUASION or by COERSION!"
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama imeshindikana kabisa kuwaongezea walimu mshahara, basi angalau madai yao halali ya malimbikizo ya mshahara, pesa za likizo na pesa za uhamisho wapewe. Hapo ndipo ulipo ugomvi wangu na serikali!
   
 10. S

  Shelisheli Senior Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ni wasaliti wa wenzao! Kama chama kinachounganisha walimu kimeitisha mgomo nchi nzima kuishtua serikali hii dhalimu wewe ukipinga msimamo huo utaitwa nani? Tumia bongo kufikiri sio kukalia.
   
 11. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,925
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  others keep on saying that chadema will change the situation..,!!mmmmmh onlg god knows coz 'everybody wants change bt nobody wants to change''bado sijashawishika kama ccm will hand over this power to their rivals in a peaceful way..
   
 12. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Van dame umeleta pumba. Huna aibu?
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi ambao hawakumchahua Kikwete mwaka 2010 hivi sasa si rais wao?
   
 14. n

  neva Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Shelisheli;Ni kweli ni wasaliti wa wenzao! Kama chama kinachounganisha walimu kimeitisha mgomo nchi nzima kuishtua serikali hii dhalimu wewe ukipinga msimamo huo utaitwa nani? Tumia bongo kufikiri sio kukalia...CHAMA KIPI UNACHOKIZUNGUMZIA NDUGU!!?? CWT ndio wakamuaji wa walimu namba moja , kwanza wanakamua sehemu ya mshahara huo mdogo wa mwalimu kila mwezi huku wakiwa tayari na vitega uchumi kadhaa bila kueleweka matumizi yake , pili,wameitisha mgomo wakati shule zinafungwa kupisha sensa, tatu, tayari kuna vuguvugu la uchaguzi mwaka huu wa CWT taifa ndio hao wanaitisha mgomo hii ni dhahiri KAMPENI zao kujirudisha tena ili kuzidi kunyonya walimu... fungukeni walimu CWT ilikua siku zote hizo ilhali taeching allowance ilifutwa miaka mingi iliyopita ndugu yangu!!??
   
 15. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Alaaaa kumbe!! Hapa hata zoezi la sensa litavurugika, kama walimu watakuwa kwenye mgomo inabidi wasihusishwe kwenye zoezi la sensa ingawa walipewa kipaumbele katika kuwa miongoni mwa watakaokuwa wanahesabu watu. Na muda wo wote waliochaguliwa wataitwa kwenye mafunzo ya sensa. Kwa vile serikali wanayoigomea ni hii hii basi wasiteuliwa katika zoezi hili maana watakuwa majumbani wanaendelea na mgomo........
   
 16. s

  sha Senior Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu shelisheli nakuunga mkono, ni wasaliti, chukulia dhana hii, je wao si wanachama wa cwt??? Je wanapomchagua raisi wao wote huwa wamempigia kura za ndio????????? Ukweli ni kwamba hata waliopiga kura za hapana aliyeshinda huwa raisi wa wote, kanusha.
  Hivyo, ndivyo hivyo kwenye migomo kura ya ndio ikishinda huo ndio huwa uamuzi wa mwisho wa wanachama wote, kwenda kinyume ni uasi - neno la mungu linasema waoga hawatauingia ufalme wa mungu, waoga hawanifai. Ukishindwa kushindana na mpinzani wako ungana naye. Hekima na busara ni bora kuliko mali nyingi.
   
 17. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Swala la kuwalazimisha wengine wasiotaka ni kuvunja katiba
   
 18. s

  sha Senior Member

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli ni wasaliti.
   
 19. s

  sha Senior Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu shelisheli nakuunga mkono, ni wasaliti, chukulia dhana hii, je wao si wanachama wa cwt??? Je wanapomchagua raisi wao wote huwa wamempigia kura za ndio????????? Ukweli ni kwamba hata waliopiga kura za hapana aliyeshinda huwa raisi wa wote, kanusha.
  Hivyo, ndivyo hivyo kwenye migomo kura ya ndio ikishinda huo ndio huwa uamuzi wa mwisho wa wanachama wote, kwenda kinyume ni uasi - neno la mungu linasema waoga hawatauingia ufalme wa mungu, waoga hawanifai. Ukishindwa kushindana na mpinzani wako ungana naye. Hekima na busara ni bora kuliko mali nyingi.
   
 20. papason

  papason JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Mkuu zubedayo!

  Na huo u van dame wako wakati wa vita kuu ya dunia ya pili kweli wewe ungeweza ku survive?

  Hata Mwenyezi Mungu anauchukia uoga!
   
Loading...