ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Kuna mgogoro mkubwa umeibuka huko wilaya ya Mbinga kati ya shule na maafisa wao. Chanzo cha mgogoro huo ni maafisa kuwataka walimu wakuu kupeleka fedha zote kwa mkurugenzi huku wakitishiwa asiyepeleka atavuliwa madaraka. Walimu wengine wanahoji uhalali wa kupeleka fedha hiyo kwa maagizo ya mdomo baadala ya barua kama iliivyozoeleka kwa taratibu za serikali. Wao maafisa wanadai kwamba wameagizwa na RAS kuchukua fedha hizo kwa kigezo cha kuendeshea michezo.
Kinachowasikitisha walimu ni utaratibu kukiukwa kwani wanafahamu kwamba katika fedha za magufuri kwa mwaka mzima kila mtoto atatumia sh. 1000 kwa ajiri ya michezo, yaani sh. 100 kwa kila mwezi wa masomo. Mpaka hivi sasa fedha ya magufuri imeshaingizwa miezi minne ina maana kila mtoto kaingiziwa sh. 400 ya michezo. Tatizo la mgogoro huo ni kwamba walimu wakuu wameambiwa wapeleke fedha yote yaani sh. 1000 ya mwaka mzima wakati fedha yenyewe mtoto ameingiziwa sh. 400 hivyo kuwalazimisha watoe fedha zote toka maeneo mengine hivyo kulazimika shule kubaki bila pesa hivyo kusababisha shule kushindwa kujiendesha na hivyo hata kifungu cha mitihani watoto watashindwa kufanya mitihani na kupewa ripoti kwani shule zote zimebaki hazina kitu.
Baada ya kuongea na walimu wakuu wa baadhi ya shule wao wamekiri kutishwa na kulazimishwa kufanya hivyo, huku wengine wakihoji kwa maafisa wao waraka unaowataka kutoa fedha ya vifungu vingine kwa ajiri ya michezo lakini pili kutoa fedha za mwaka mzima ili hali serikali imetoa fedha kwa miezi mitano tu . Hakuna majibu wanayopewa zaidi ya kutishwa na kuanzia jana kumekuwa wimbi kubwa la walimu wakuu kupitisha mihtasari ya kutoa fedha hizo huku hiyo mihtasari ikiandikwa activities za uongo ili kusaidia upatikanaji wa fedha hizo.
A fisa elimu halmashauri ya mji anafahamu dili hilo . Walimu wanahoji kama kweli hayo ni maagizo halali kwa nini wasifuate uraratibu wa serikali wa kuwaandikia barua baadala ya kutoa maagizo ya mdomo., vyombo vinavyohusika TAKUKURU, TISS na vinginevyo vifuatilie suala hilo kwani hayo ni matumizi mabaya ya ofisi.
walimu wa kawaida wamegoma kuweka sahihi zao kwenye mihtasari inayopitishwa tangu jana lakini walimu wakuu wamefoji sahihi za uongo za walimu ili kufanikisha upatikanaji wa fedha hiyo .