Walimu wa mziki wanahitajika

Walimu wa mziki wanahitajika

GK Francis

Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
17
Reaction score
0
C:\Users\KUBELELA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg
EBENEZA MUSIC TRAINING CENTRE (EMTC) [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 525"]
[TR]
[TD="width: 701"] Mobile: +255 752 268 396 P. O. Box 10, Itigi E-mail:ebenezamusictraining@yahoo.com
+255 787 895 473 TANZANIA. www.facebook.com/Ebenezamusictraining/ [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
28/09/2015
MAELEZO

Ebeneza Music Training Centre (EMTC) ni kituo kinachotoa mafunzo ya Mziki kwa vijana ili kuwawezesha kujiajiri kupitia fani ya mziki. Kituo hiki kiko katika Mji wa Itigi wilaya ya Manyoni , Mkoa wa Singida na kinatarajia kuanza rasmi mafunzo hayo mara baada ya kupata walimu wa mziki. Hivyo Mkurugenzi wa EMTC anakaribisha maombi kwa wataalamu katika fani ya mziki kama ifuatavyo:
NAFASI: MKUFUNZI WA MZIKI –NAFASI 2
MKATABA: MIEZI 8
Sifa za Mwombaji
§ Awe na Shahada au Diploma katika fani ya mziki kutoka chuo chochote kinachotambuliwa.
§ Awe na uelewa nadharia na vitendo kuhusu mziki
§ Awe na uwezo wa kufundisha kinanda (Keyboard), magitaa, na sauti kwa nadharia na vitendo
§ Awe na moyo wa kujituma katika kutekeleza majukumu yake kwa kadri itakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa mafunzo
NAFASI: MKUFUNZI MSAIDIZI WA MZIKI –NAFASI 1
MKATABA: MIEZI 8
Sifa za Mwombaji
§ Awe na uzoefu wa kupiga kinanda (Keyboard), gitaa na drums
§ Awe na uwezo wa kufundisha kinanda (Keyboard), gitaa au drums kwa vitendo
§ Mwenye cheti cha mziki atapewa kipaumbele
Kwa yeyote mwenye sifa atume maombi atume maombi pamoja na maelezo binafsi (CV) ikiwa na mawasiliano yako kwa Barua pepe hapo juu.
NB. Hakuna gharama yoyote atakayotozwa mwombaji isipokuwa atatakiwa kugharimia usafiri wake binafsi kuhudhuria mahojiano (interview)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom