Walimu tisa waishi kwenye vyumba vitatu

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
Katika hali inayochochea msongo wa mawazo, walimu tisa wamejikuta wakiishi katika vyumba vitatu vya nyumba moja kutokana na uhaba wa nyumba.

Kufuatia hali hiyo, Baraza la Madiwani la Sengerema mkoani Mwanza limemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwatafutia nyumba mara moja walimu walimu hao.

Walimu wanaodaiwa kuishi kwenye nyumba moja yenye vyumba vitatu ni wa Shule ya Msingi Soswa wilayani hapa mkoani Mwanza baada ya kuripoti eneo la kazi na kukuta uhaba mkubwa wa nyumba za walimu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Diwani wa Kata ya Bulyaheke, Bageti Ngele kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata yake ambapo alisema licha ya kuwepo mafanikio makubwa ya miradi, kata hiyo inakabiliwa na ukosefu wa nyumba za walimu kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari, akitoa mfano wa walimu tisa wa shule ya msingi Soswa kuishi kwenye nyumba moja.

Ngele alidai hatua hiyo imekuwa ikiwaathiri walimu hao kisaikolojia na kuwa vigumu kupunguza tamaa ya mwili itokanayo na tendo la ndoa licha ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kuishi yeye na familia yake ndani ya nyumba hiyo ambayo hata hivyo haina dari.

Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mathew Lubongeja alimwagiza Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Juma Mwajombe kuhakikisha walimu hao wanaondolewa kwenye nyumba hiyo haraka wakati serikali ikijipanga kuondoa tatizo hilo.

“Kutokana na unyeti wa suala hili…mkurugenzi ninakuagiza uhakikishe walimu hao wanaondoka haraka kwenye nyumba hiyo ili ibaki idadi inayokubalika kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha walimu hao kuathirika kisaikolojia…hii ni hatari sana,”alisema Lubongeja.

Aidha alisema jitihada za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha shule hiyo inaongezewa majengo ya nyumba za walimu haraka kwa kutumia fedha za serikali badala ya kuendelea kusubiri michango ya wananchi katika kutekeleza miradi hiyo.

Kaimu mkurugenzi huyo aliahidi kulishughulikia haraka suala hilo kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa Umma ili kuondoa adha inayowakabili walimu hao.

Alisema hatua hiyo inaweza kuathiri kiwango cha utoaji elimu kwa wanafunzi kutokana na walimu hao kuishi kwa misongo ya mawazo.
 
nchi haijengwi na mafisadi bali inajengwa na wananchi wenye nia na uzalendo wa kweli na si uzalendo wa majukwaani
 
Back
Top Bottom