WALIMU: Mgomo HATARI Kuliko Mingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WALIMU: Mgomo HATARI Kuliko Mingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Aug 6, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  View attachment 60991 ..... View attachment 60992 ... View attachment 60993

  WAALIMU: mgomo HATARI zaidi Kuliko mingine


  Katika Utumishi wa serikali kuna kada mbalimbali zikiwemo Jeshi, Uuguzi, watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa pamoja na mashirika yake ya Umma.

  Mgomo wa Walimu ndio unaoongoza kwa uwezo mkubwa wa kutunisha misuli yake na kuleta maafa makubwa sana na athari ambazo si rahisi kuzibika kama ukiachiwa uendelee kwa zaidi ya wiki moja.
  Kwa kifupi tuchambue migomo ya sekta hizi tukioanisha na mgomo wa sekta ya Elimu ndani ya nchi

  JESHI:

  Kwa Chambuzi zangu, Mgomo wa Jeshi, Mathalan Jeshi la Magereza, Polisi na Jeshi la wananchi. Wakigoma au wakaacha kufanya kazi zao za kila siku, hasara au madhara yatayotokana na mgomo wao yanategemea ustarabu wa jamii Husika, na nchi husika. Kwa upande wa Jeshi, Mipaka ya Ulinzi wa nchi na nchi kwa sasa ni Jukumu ya Umoja wa Kimataifa. Hata nchi yako ikivamiwa ni suala la jeshi la Umoja wa mataifa linaloundwa na nchi washiriki kwenye mabara husika na ndio wenye dhamana ya Kumtimua mvamizi. Hivyo kwenye ulimwengu wa saa Jeshi la Ulinzi sanansana ni chombo cha kukodiwa na kukodisha.

  Magereza wakigoma kuna tutarajie kundi kubwa la wafungwa maskini hao ambao wengi wamefungwa kwa wizi wa kuku na shati, wengine wamebambikiziwa kesi, wengine husuda tu, na wengine na kakundi kadogo sana ambo kweli wamfungwa kwa makosa halali, wote hwa watakuwa HURU, huku watu waliotafuna keki ya taifa na kukwimba mamilioni na kufanya mauaji mengi ya kutisha wakiendelea kula bata kwenye taifa letu huru kabisa.

  Tukijumlisha na mgomo wa Polisi, Nchi yetu kwa sasa sidhani kama kuna raia anayejivunia Jeshi la Polisi. Raia wengi wanajilinda wenyewe kwa Ulinzi shirikishi na wanalipia ulinzi huo kwa fedha zao. Jeshi la Polisi limekuwa adui kwa wananchi wake. Mtu akiwa na shida ya ain yoyote akikimbilia polisi anavuna machungu, kero na usumbufu wa kila aina. Polisi wetu hawana rekodi ya kukamata jambazi, ukivamiwa usiku, kwanza wanakuja muda mrefu baada ya tukio, na ni mahiri kwelikweli wa kuandika taarifa za tukio na kutimua zao. Barabarani napo watu watakuwa free ku-drive pasipo mikonomikono na kuombwa vijisenti all ways. So jeshi la Polisi kw Tanzania Likigoma Kutakuwa na Uhuru sana kwa raia.. kero wakati wa usiku zitashughulikiwa na Sungusungu, Ulinzi shirikishi na makumi ya makampuni ya Ulinzi yaliyopo.
  Kwa Upande wa watumishi hao wa jeshi , mgomo huo utaendelea na wao bila kuathiri tabaka jingine la jamii.

  UUGUZI:

  Sekta hii nayo kwa upande wake ikigoma kuna madhara makubwa ya kitabibu ambayo yataathiri kipande cha jamii hasa kile kinachopitia nyakati za maradhi huku upande mkubwa wa jamii nyingine ukiwa Shwari. Kutokana na wigo mpana wa sekta ya matibabu, waathirika ambao ni wagonjwa wanaweza kujihifadhi kwenye wingi wa vituo na hospitali za binafsi zilizopo, ingawa gharama kwa baadhi ya wagonjwa wasio na uwezo mzuri zitawasumbua, lakini kuna ahueni kwamba walau kuna hospitali za binafsi ndani ya miji mikubwa na vijijini pia. Hivyo makali ya mgomo wa sekta hii kwa watumishi wa serikali walau unaweza kudhibitiwa kwa kiasi Fulani.

  MGOMO KWA WATUMISHI WA SERIKALI KUUNA MITAA.

  Kwa ujumla madhara ya mgomu huu ni kuchelewesha shughuli za kimaendeleo ambazo kwa jamii yetu sio tu hazionekani bali zimezimika kwa muda mrefu. Na pia vievile mgomo huu ni moja kati ya migomo isiyo na mshiko .

  MGOMO WA WAALIMU.

  Mgomo wa waalimu wa kada yoyoye huleta madhara makubwa sana ambayo si rahisi kuyadhibiti. Walimu wakigoma sekta ya Elimu ambayo huongozwa na mitaala na mitala huongozwa na Muda wa majira ya mwaka. Mgomo wa waalimu huathiri na kusimamisha mtaala wa taaluma wakati muda ukiendelea kuyoyoma. Hakuna mrahama (replacement ) ya Muda, mtaala ukipita umepita, kipindi kikiondoka hakirudi tena. Si rahisi kurudia mtaala. Mgomo wa waalimu hukatili taaluma ya wanafunzi, na kama ukidumu kwa zaidi ya wiki, Mtaala utaharibika. Na kama mfumo wa mtaala umeharibika, lazima uanze upya. Hii ina maana serikali inaahirisha masomo ya wanafunzi kwa mwaka mzima na kuanza tena upya. Hii ina maana wale wanaopanda na elimu ya juu, lazima liwepo Gap la mwaka mzima na wale wanaotaraia kuanza shule watawajibika kuahirisha na kurundikana baada ya mwaka. Si tu kuathiri wanaodahiriwa bali pia itaathiri wale wataoendelea na masomo kwenye private sc, maana italazimika ama wakae mwaka mzima wakisubiri kada nyingine ya mfumo wa serikali au wahitimishe taaluma zao kikatili.
  Mgomo wa waalimu huleta Athari kubwa za kisaikolojia kwa wanafunzi ambao watalazimika kuhaha wakitafuta endelezo la elimu zao, si kwa wanafunzi tu bali hata wazazi wataingia kwenye wakati mgumu wa kulazimika kupanga jinsi ya kuwaendeleza watoto wao lakini pia kubadoilisha mtiririko wa mipango yao ya kifamilia.
  Mgomo wa waalimu ni mgomo wa chi nzima na wadau wa kada zote. Unawaathiri madaktari, wanajeshi, watumishi wa serikali kuu na mitaa, wanasiasa, watumishi wa kada binafsi na wazazi kwa sababu kwa namna yoyote lazima watoto wao watakuwa kwenye mfumo wa kitaaluma hivyo itawakera na kuwasumbua sana. Mwalimu ni mtu wa Muhimu sana.
  Mgomo wa waalimu huumiza kila sekta, Hatakama serikali italazimisha waalimu kuendelea na kazi zao bila kugoma pasipo kuwatimizia mahitaji yao, watafanyika vyombo hatari sana kwenye sahani la Elimu. Ni hatari mwalimu ambaye hakuridhishwa na mwajiri wake (discontented) Kutoa elimu kwa mwanafunzi. Lazima ataharibu na kuathiri baadae(future) ya watoto wa taifa hili la keshokutwa kama si la kesho.
  Mgomo wa waalimuni janga la Taifa lolote makini, ila taifa la mabaradhuli, wazee wa liwalo na liwe, wasiojali utaifa wala wataifa, kwao ni POTELEAMBALI.

  View attachment 60997
   
 2. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu inakwambia Liwalo na liwe kama madaktari , wauguzi na walimu wakigoma. Kama wabunge wakigoma, basi serikali itahaha usiku kucha kutekeleza hayo madai yao kwa kisingizio eti "maendeleo ya nchi yataathirika"! Serikali yet bana!!
   
 3. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu wale walioandamana wakamwambia Mzee Nyerere kwamba Mkoloni alikuwa bora kuliko Serikali za watu weusi nafikiri walikuwa sahihi sijui wewe unaonaje?
  Hata wale waliosema Africa is a dark continent,pia nasema kwa mazingira yetu walitabiri kwa usahihi.Wewe unaonaje?
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Subirini matokeo ya mtihan wa kidato cha II na IV mwakani
   
 5. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  achana na serikali kiziwi, kipofu yenyewe inajua kubwabwaja tu,
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  ushauri wangu kwa walimu.EITHER MGOME MPAKA KIELEWE AMA MPIGE KAZI KWA KWENDA MBELE.KItendo cha kugoma kimya kimya ni UOGA na NI WIZI na NI UNAFIKI WA KUTUPWA...Hakuna maana yeyote ya kugoma kimya kimya.MTAKUWA HAMUWATENDEI WATOTO WA Wakulima hali yao ni HIYO KWANGU NI DHAMBI KUBWA...kama hamuendi darasani waambieni wakae home sio kuwapotezea muda..natambua mna hoja ya msingi ya madai yenu ila approach ya kugoma kimya kimya NI DHULUMA.DHAMBI.WOGA WA HALI YA JUU SANA NA NI UNAFIKI MKUBWA NA NI KINYUME NA MAADILI YA KAZI YENU...
   
 7. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,401
  Likes Received: 1,525
  Trophy Points: 280
  ........wagowagomee walalahoi wenzao, watoto wangu wako Uganda. No body cares!!!!!!!!!!!
   
 8. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ..
  but ni kweli sometimes.. who cares.. who cares.. tunaumizana wenyewe
   
 9. D

  Deo JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Matokeo makubwa ya mgumo uliozimwa kwa nguvu tena kwa kejeli na matusi kwa waalimu ni kifo cha mende kwa sisiemu. Waalimu wengi wa huku kwetu kijijini ni watu muhimu sana, tunawaheshimu, tunawasikiliza. Waliipenda chama chao cha sisiemu ambacho leo kimewageuka. Wale wanaozungumza na sisi wameapa sasa ni mwisho wa chama hiki, hasira inapanda zaidi kwa vile hata ile posho ya sensa wamenyimwa.
  Subirini muone.
  Zaidi nafasi zote za sisiemu wananchi wamekataa kuchukua fomu. Unaombwa ugombee nafasi yoyote lakini hakuna anayetaka.
  Sisiemu unaenda wapi mama yangu? Utafia kweli mikononi mwa jk asiyekupenda?
   
 10. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eng, Mimi kwa maoni yangu sikuwa nadhani hata kama tungefikia hatua ya Kujadili mgomo upi ni hatari kuliko mwingine kwa sababu migomo yote inamatokeo hasi... Hapa ni tuiwajibishe serikali iliyoshindwa kutatua matatizo ya taifa kwa njia ya majadiliano hadi inakuwa migomo

  SULUHISHO: Tuendelee kuelimishana wenyewe kwa wenyewe hasa vijijini ili kuongeza uelewa (awareness) wakati huo huo serikali ikizidi kutupandisha hasria kwa mambo mbali mbali kama mishahara midogo hafu wanaleta sheria ya mafao kuchukua mpaka 55yrs, kutumia mabavu ya vyombo vya dola kama mahakama,kuruhusu ajali kama za mv spagit, mabomu ya mbagala, kukosa huduma za jamii kama madawa hospitalini na vitabu mashuleni

  TUKISHAFIKIA HATUA YA KUTORUDI NYUMA (POINT OF NO RETURN) KISAIKOLOJIA.. HATUTASUBILI MTU YOYOTE YULE ATUAMBIE.. WENYEWE TUTAENDA MAGOGONI KUMCHOMOA MTU.
   
Loading...