Kuna ndugu yangu mmoja hapa Arusha ambaye anafanya kazi ofisi za jiji amenidokeza walimu wote, walioanza kazi mwaka 2011 mpaka mwaka huu 2014 ambao kimsingi wamesha maliza miaka mitatu kazini hivyo wanadeserve kupandishwa daraja, serikali imesha anza dana dana kua eti mwaka wao unaanza mwaka 2012 kwa kua ndo mwaka wa kuthibitishwa kazini. Hivyo miaka mitatu kwa mujibu wa serikali miaka 3 itakua mwaka 2015 ndio mwaka wa kupandishwa daraja..ONYO: Nawaambia mapema msijaribu, intake ya mwaka huo ni hataree muulizeni aliyekua mkurugenzi Estomii Chang'a aliyejaribu kumeza fedha za substitutional allowance za walimu mwanzôn mwa mwaka 2011.